Pata taarifa kuu

Burma: Umoja wa Mataifa walaani "uhalifu dhidi ya binadamu" tangu mapinduzi

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya mapinduzi nchini Burma, Umoja wa Mataifa umeshutumu jeshi la Burma kwa "uhalifu dhidi ya binadamu". Katika ripoti yake ya hivi punde, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa inaripoti ukiukwaji mkubwa uliofanywa dhidi ya raia tangu Februari 1, 2021 na inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchunguza janga hili ambalo limepuuzwa tangu mwanzo wa vita nchini Ukraine.

Serikali ya Burma inalenga kunyamazisha vuguvugu linalounga mkono demokrasia, tangu ilipochukua mamlaka. Hapa, waandamanaji dhidi ya utawala wa kijeshi, huko Ayadaw, wilaya ya Monywa, Februari 13, 2022.
Serikali ya Burma inalenga kunyamazisha vuguvugu linalounga mkono demokrasia, tangu ilipochukua mamlaka. Hapa, waandamanaji dhidi ya utawala wa kijeshi, huko Ayadaw, wilaya ya Monywa, Februari 13, 2022. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kiwango cha kutisha na visa vingi vya ukiukaji wa sheria za kimataifa vinavyofanyiwa raia wa Burma vinahitaji jibu thabiti, linaloungwa mkono na lenye suluhu," Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Michelle Bachelet, amesema katika taarifa.

Ofisi ya Kamishna Mkuu inashutumu jeshi la Burma kwa kujihusisha na "ukiukaji wa jumla na ulioenea na ukiukwaji wa haki za binadamu". Baadhi ya ukiukaji huu "unaweza kuhusishwa na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu", umebaini Umoja wa Mataifa, ambao una tabia ya kuziachia mahakama kuamua.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR), Ravina Shamdasani, "Kwa kweli tumeweza kutambua kuwepo kwa mfumo wa operesheni katika mwaka uliopita, ambao unaonyesha kuwa kulikuwa na mashambulizi  ya jumla, uratibu na mipango, na kwamba kulikuwa na dalili za wazi kuwa kuliripotiwa uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu”:

Jeshi la Burma linaendelea na ukiukaji wake mkubwa na wa utaratibu wa haki za binadamu na tunabaini kwamba baadhi ya ukiukaji huu unaweza kutambuliwa kama uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Wanajeshi wa Burma hushambulia maeneo ya makazi na kuwalenga raia, ambao hupigwa risasi kimakusudi, wakati mwingine kuchomwa moto wakiwa hai, kuzuiliwa kiholela, kuteswa au kutumiwa kama ngao za binadamu. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za haraka kuwawajibisha wahusika wa ukatili huu na kukomesha ghasia hizo. Hatua hizi za haraka zinaweza kuchukua namna ya vikwazo, ikiwa ni pamoja na kusitisha kulipa silaha jeshi la Burma, hadi wale waliohusika wawajibishwe, ikiwa ni pamoja na mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.