Pata taarifa kuu
MYANMAR-HAKI

Aung San Suu Kyi aukumiwa miaka mingine minne jela

Mahakama nchini Myanmar imemhukumu jela aliyekuwa kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi miaka mingine minne, kwa kosa la kumiliki na kuingiza vifaa vya mawasiliano- walkie-talkies kinyume cha sheria lakini pia kuvunja masharti ya kupambana na Covid-19.

Mmoja wa waandamanaji akionyesha picha ya kiongozi wao Aung San Suu Kyi anayezuiliwa jela.
Mmoja wa waandamanaji akionyesha picha ya kiongozi wao Aung San Suu Kyi anayezuiliwa jela. AP - Sakchai Lalit
Matangazo ya kibiashara

Hukumu hii ya pili inakuja, baada ya Suu Kyi kupewa hukumu nyingine mwezi Desemba mwaka uliopita, iliyopunguzwa hadi miaka miwili na sasa hukumu zote mbili, ni miaka sita jela, huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda hatimaye akafungwa akapewa kifungo cha maisha jela.

Hukumu dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Mynmar, kumeendelea kushutumiwa na mataifa ya Magharibi kwa kile wanachosema yamechochewa kisiasa.

Mwezi Februari mwaka uliopita, Aung San Suu Kyi baada ya chama chake cha National League for Democracy kushinda uchaguzi wa wabunge, alikamatwa na wanajeshi na kuzuiwa nyumbani, kabla ya kufunguliwa mashtaka mbalimbali.

Jeshi nchini Myanmar limeendelea kudai kuwa, uchaguzi wa mwaka uliopita, haukuwa huru na haki, kinyume cha ripoti ya waangalizi huru waliosema, uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.

Baada ya hatua hiyo ya jeshi kuchukua madaraka na kumkamata kiongozi huyo wa kiraia, kulizuka maandamano ambayo yamesababisha vifi vya zaidi ya watu 1,303 na wengine zaidi ya Elfu 10 kukamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.