Pata taarifa kuu

Burma: ASEAN yapaza sauti dhidi ya utawala wa kijeshi

Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia inapaza sauti dhidi ya Burma, bila kuweka vikwazo kwa serikali ya kijeshi. Wakuu wa diplomasia wa nchi wanachama wa umoja huo, waliokutana huko Phnom Penh, wamehimiza mamlaka ya Naypyidaw kutumia makubaliano ya kumaliza mzozo huo katika nukta tano zilizokubaliwa miezi mitatu baada ya mapinduzi kati ya serikali ya kijeshi na Asean.

Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burma, hapa ilikuwa Juni 21, 2021 huko Moscow, Urusi.
Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burma, hapa ilikuwa Juni 21, 2021 huko Moscow, Urusi. AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yao ya pamoja, wanadiplomasia hao wamesema "wamesikitishwa sana na maendeleo finyu na ukosefu wa dhamira ya serikali kuu katika kutekeleza makubaliano hayo yenye vipengele vitano". Makubaliano ambayo yalitaka, pamoja na mambo mengine, kukomesha ghasia, kuanza mazungumzo na vyama vya upinzani na kumteua mjumbe maalum kutoka ASEAN katika jukumu la upatanishi.

Baada ya kutengwa katika vikao vya kimataifa, Burma haikualikwa kwenye mkutano wa kilele wa Phnom Penh ikipignwa na jumuiya hiyo dhidi ya kunyongwa kwa wapinzani wa kisiasa hivi karibuni. ASEAN haijapanga katika hatua hii kumtenga mshirika wake kutoka jumuiya hiyo, uchunguzi mpya kuhusu suala hilo utafanyika katika mkutano ujao wa kilele mnamo mwezi wa Novemba.

Katika ishara kwamba baadhi ya nchi zinakosa subira, Waziri Mkuu wa Cambodia, Hun Sen alionya Jumatano Agosti 3 kwamba hukumu mpya za kunyongwa kwa wafungwa zinaweza kulazimisha jumuiya hiyo kufikiria upya makubaliano hayo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya wafungwa 100 kwa sasa wanasubiri kunyongwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.