Pata taarifa kuu

Burma: Serikali ya kijeshi yaongeza muda wa hali ya hatari kwa miezi sita

Tarehe 1 mwezi huu wa Februari inaadhimishwa miaka miwili tangu jeshi kunyakua mamlaka nchini Burma, likimfunga nyota na kiongozi wa demokrasia Aung San Suu Kyi na kuzusha vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya zaidi ya 2,800 na raia 13,000 wakifungwa jela. Katika siku hii ya kumbukumbu, utawala wa kijeshi umeongeza muda wa hali ya hatari.

Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burma, wakati wa mkutano wa Baraza la kitaifa la ulinzi na usalama mnamo Jumanne, Januari 31, 2023 huko Naypyidaw.
Jenerali Min Aung Hlaing, mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burma, wakati wa mkutano wa Baraza la kitaifa la ulinzi na usalama mnamo Jumanne, Januari 31, 2023 huko Naypyidaw. AP
Matangazo ya kibiashara

Baraza la kitaifa la ulinzi na salama, linaloundwa na maafisa wa utawala wa kijeshi, limekubali siku ya Jumatano kuongeza muda wa hali ya hatari nchini Burma kwa miezi sita, vyombo vya habari vya serikali vilmetangaza. Ombi la kiongozi wa utawala wa kijeshi Min Aung Hlaing la kuongeza muda wa hali ya hatari, lililotangazwa wakati jeshi lilipindua serikali ya Aung San Suu Kyi mnamo Februari 2021, limekubaliwa, shirika la utangazaji la serikali MRTV limesema.

Kaimu Rais Myint Swe ameongeza kuwa "mamlaka ya kujitawala ya nchi kwa mara nyingine tena yamehamishiwa kwa Amiri Jeshi Mkuu". Muda wa hali ya hatari ulipaswa kumalizika mwishoni mwa mwezi Januari, lakini siku ya Jumanne Baraza la kitaifa la ulinzi na usalama lilikutana kujadili hali ya taifa na kuhitimisha kuwa "bado haijarejea katika hali ya kawaida".

Min Aung Hlaing pia alithibitisha kuwa "serikali itafanya kazi kuandaa uchaguzi katika mikoa yote ya nchi ili watu wasipoteze haki zao za kidemokrasia".

Huko Rangoon, sensa ya watu inakaribia kukamilika, na utawala unachukua fursa hiyo kuangalia ikiwa familia zinampa hifadhi mpinzani mmoja au wawili wa kisiasa. Maisha yameanza tena kwa njia fulani, bei ya chakula imeongezeka mara mbili katika miaka miwili, lakini mishahara imebaki vile vile. Maadhimisho ya mapinduzi yamejawa na huzuni, na sehemu ya watu wameamua, kama mwaka jana, kubaki nyumbani - aina ya maandamano ya kimya kimya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.