Pata taarifa kuu

Burma: Utawala wa kijeshi wafuta LND, chama cha Aung San Suu Kyi

Tume ya uchaguzi ya Burma, iliyoundwa na utawala wa kijeshi, imetangaza kuvunjwa kwa National League for Democracy (NLD), chama cha Aung San Suu Kyi, Jumanne Machi 28. NLD itajikuta kimefutwa moja kwa moja kwenye orodha ya vyama vya siasa nchini Burma kuanzia siku ya Jumatano, televisheni ya taifa imesema.

Aung San Suu Kyi mjini Tokyo, Japani tarehe 9 Oktoba 2018.
Aung San Suu Kyi mjini Tokyo, Japani tarehe 9 Oktoba 2018. REUTERS - POOL New
Matangazo ya kibiashara

 

Tangazo hilo linakuja baada ya kurefushwa kwa muda wa hali ya hatari, zaidi ya miaka miwili baada ya mapinduzi ambapo jeshi lilipindua serikali ya kiraia na kumhukumu mkuu huyo wa zamani wa serikali kifungo cha miaka 33 jela.

Utawala wa kijeshi umekiangusha chama kimoja pekee chenye uwezo wa kukibadilisha hali katika uchaguzi mpya. Uchaguzi ujao, unaotakwa na wanajeshi wa Burma kuhalalisha mamlaka yao na kukisushia lawama chama cha NLD wa kutoa wito wa kususia shughuli za serikali, wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaiathiri nchi hii. Ikiwa masharti yote yatatimizwa, uchaguzi wa wabunge unaweza kufanywa katika mazingira bora zaidi mwezi Novemba mwaka huu.

NLD ni moja ya vyama vikuu vya kisiasa, mpinzani wa kihistoria wa utawala wa kijeshi tangu kuundwa kwake mnamo 1988, kufuatia uasi dhidi ya serikali ya kijeshi. Chama hiki, kilichoanzishwa na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 1991, Aung San Suu Kyi, kwa kiasi kikubwa kilishinda uchaguzi wa wabunge mwaka wa 2015 na 2020.

Baada ya mapinduzi ya kijeshi, chama kilivunjika. Aung San Suu Kyi na mshirika wake wa karibu walipokea, katika kesi zisizoeleweka, vifungo vizito gerezani; viongozi wengi waliochaguliwa waliuawa katika wiki zilizofuata mapinduzi ya kijeshi, na wengine wanaishi mafichoni au uhamishoni.

Vyama vya kisiasa nchini Burma vina hadi Jumatano Machi 29 kutimiza masharti magumu na mapya kwa baadhi, ili kuona hadhi yao ikiongezwa au kufutwa kiotomatiki. Ili chama kiendelee kuwa hai, lazima:

  • kuajiri wanachama 100,000 kabla ya siku 90 baada ya usajili; hapo awali ilihitaji wanachama 1,000 pekee
  • kufungua akaunti yenye amana ya angalau kyat milioni 100, ambayo ni takriban $35,000 katika soko la sasa la ubadilishaji fedha (hii ni sheria mpya)
  • kufungua ofisi katika angalau nusu ya kanti 330 ndani ya siku 180 za usajili (hii pia ni sheria mpya)
  • kushiriki katika angalau nusu ya majimbo ya uchaguzi nchini kote; kabla, ilichukua majimbo matatu tu
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.