Pata taarifa kuu

Waziri wa ulinzi wa China akaribisha uhusiano wa 'nguvu' na Moscow

Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu amekaribisha uhusiano wa "nguvu" na Moscow Jumapili Aprili 16 wakati wa mkutano na Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Kremlin. "Tuna mahusiano yenye nguvu sana, ambayo yanapita zaidi ya ushirikiano wa kijeshi na kisiasa wa enzi ya Vita Baridi" na ni "imara sana", amesema wakati wa mkutano huu uliorushwa kwenye televisheni ya Urusi, kulingana na tafsiri yao.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu wakikutana huko Moscow, Urusi, Aprili 16, 2023.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Waziri wa Ulinzi wa China Li Shangfu wakikutana huko Moscow, Urusi, Aprili 16, 2023. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Ameongeza kuwa uhusiano kati ya Urusi na China "tayari umeingia katika enzi mpya". “Hii ni ziara yangu ya kwanza nje ya nchi tangu niingie madarakani kama Waziri wa Ulinzi. Nimechagua Urusi hasa, ili kusisitiza hali maalum na umuhimu wa kimkakati wa uhusiano wetu wa nchi mbili," Li Shangfu amebainisha.

Wakati wa mkutano huu, ambao pia ulihudhuriwa na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu, Vladimir Putin amepongeza ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili. "Tunafanya kazi kwa bidii kupitia idara za kijeshi, kubadilishana habari muhimu mara kwa mara, tunashirikiana katika uwanja wa ushirikiano wa kijeshi na kiufundi na kufanya mazoezi ya pamoja," Vladimir Putin amesema.

"Bila shaka hili ni eneo jingine muhimu ambalo linaimarisha asili ... ya uhusiano wetu," ameongeza. Ziara hii ya Li Shangfu nchini Urusi, inayotarajiwa kudumu hadi Aprili 19, inakuja baada ya ile ya Rais Xi Jinping wa China mwezi Machi mjini Moscow. Wakati wa mkutano huu, Vladimir Putin na Xi Jinping walionyesha uelewa wao mzuri, wakijifanya kama washirika wa kimkakati walioazimia kupinga utawala wa Marekani. Tangu kuanza kwa mzozo huo, Beijing imejitangaza kuwa haina upande wowote inayoegemea, bila hata hivyo kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Xi Jinping hajawahi kuzungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.