Pata taarifa kuu

Mgogoro wa kiuchumi: Sri Lanka kusafirisha hadi tumbili 100,000 nchini china

Kwa miezi kadhaa, Sri Lanka imekuwa ikikabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi katika historia yake na iko katika hali ya benki na makampuni yake kukaribia kufilisika. Ili kukabiliana na hali hiyo, nchi hiyo ndogo ya visiwa katika Bahari ya Hindi inazingatia suluhisho ambalo halijawahi kushuhudiwa: hadi tumbili 100,000 , spishi ya tumbili wa kawaida, zinaweza kuuzwa nje ya nchi.

Spishi hii ya tumbili iko kwenye orodha nyekundu ya Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira ya Viumbe Vilivyo Hatarini.
Spishi hii ya tumbili iko kwenye orodha nyekundu ya Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira ya Viumbe Vilivyo Hatarini. AFP - INA FASSBENDER
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya mbuga za wanyama elfu moja za China zimetoa ombi hili kwa serikali ya Sri Lanka. Na hata kama kiasi kilichopendekezwa bado hakijajulikana, kamati inayosimamia faili tayari imeteuliwa na Wizara ya Kilimo ya Sri Lanka. Shughuli hiyo inashangaza: Spishi hii ya tumbili iko kwenye orodha nyekundu ya Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka. Na Sri Lanka inapiga marufuku karibu mauzo yote ya wanyama.

Lakini nchi hii iko tayari kuchukuwa hatua ya kipekee ya kujaza fedha hazina ya serikali, hasa kwa vile sheria ya Sri Lanka hailindi spishi hii ya tumbili. Kisiwa hicho kinasemekana kuwa na tumbili milioni mbili hadi tatu. Kutokana na tumbili hawa kuwepo kila mahali, anaonekana kuwa mnyama asiyefa na mharibifu. Wanaharibu mazao, wanaingia vijijini kutafuta chakula na wakati mwingine wanashambulia raia.

Wakfu wa Mazingira unapaza sauti ukiulizwa maswali kadhaa: je, tumbili hawa wanauzwa kwa ajili ya nyama yao? Kwa utafiti wa matibabu? Kulingana na shirika hili la haki za wanyama, si haki kutaka kufutilia mbali tumbili huyo mdogo wakati ukuaji wa miji na upanuzi wa kilimo unaharibu makazi yake ya asili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.