Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

India yaipa ndege ya uchunguzi Sri Lanka wakati meli ya utafiti ya China ikiwasili

India ilitoa, Jumatatu, Agosti 15, ndege ya uchunguzi wa baharini kwa Sri Lanka ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Chombo hicho kilitua Siku ya Uhuru wa India, lakini pia siku moja kabla ya kuwasili nchini Sri Lanka kwa meli ya China ambayo India inahofia uwezo wake wa kijasusi. Meli hiyo ilitia nanga Jumanne asubuhi katika bandari ya Hambantota.

Hambantota (Sri Lanka): balozi wa China huko Colombo alikuja kupokea meli ya utafiti ya China, ambayo iliwasili Agosti 16 kwenye bandari ya Hambantota, ikidhibitiwa na China. Ziara ambayo India inalaani.
Hambantota (Sri Lanka): balozi wa China huko Colombo alikuja kupokea meli ya utafiti ya China, ambayo iliwasili Agosti 16 kwenye bandari ya Hambantota, ikidhibitiwa na China. Ziara ambayo India inalaani. AFP - ISHARA S. KODIKARA
Matangazo ya kibiashara

"Usalama wa India na Sri Lanka unaimarishwa na kuelewana kwa ushirikiano. Mchango huu ni mchango wa hivi punde wa India katika kwa ushirikiano huo,” amesema Gopal Baglay, Kamishna Mkuu wa India nchini Sri Lanka, katika kambi ya kijeshi karibu na mji wa Colombo.

Chombo hicho, Dornier 228 kilichotengenezwa nchini India, kimetolewa kwa uchunguzi wa baharini na pwani. Kufuatia mzozo wa muda mrefu na mbaya wa kiuchumi, vikosi vya majini vya Sri Lanka haviwezi kutekeleza kazi yao.

India ndio mwanzilishi wa Kongamano la Usalama la Colombo, linalojumuisha Sri Lanka, Maldives na Mauritius na linaangazia usalama wa baharini na usalama wa mtandao. Mnamo mwaka 2015, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alizindua mpango wa "Usalama na Ukuaji kwa Wote katika ukanda huo", ambao ulijumuisha mchango wa ndege hii.

Kufuatia hali hii ya ushirikiano China imekuwa ikifanya vitisho, huku ikiimarisha uwepo wake wa kijeshi na kibiashara karibu na maji ya India na hasa huko Sri Lanka. Mchango wa India kwa ndege hii, siku moja kabla ya kuwasili katika bandari ya Hambantota (Jumanne hii) meli ya utafiti ya China, kunaonyesh vita vya ushawishi kati ya chi hizi mbili vigogo wa Asia nchini Sri Lanka. Kulingana na idara ya ujasusi ya India, meli hii inaweza kutumika kufuatilia satelaiti na kufanya ujasusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.