Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Sri Lanka kuipokea meli ya China inayoshukiwa kuwa ya kijasusi, India yapandwa na hasira

Serikali ya Sri Lanka imeruhusu meli ya utafiti ya China kuegesh kwenye bandari kubwa katika kisiwa hicho licha ya wasiwasi kutoka India kwamba meli hiyo inaweza kupeleleza mitambo ya kijeshi huko New Delhi, maafisa wamesema.

Meli ya Chian, Yuan Wang 5 imeidhinishwa na mamlaka ya baharini ya Sri Lanka kuweka nanga katika bandari ya Hambantota, kaskazini mwa kisiwa hiki katika Bahari ya Hindi.
Meli ya Chian, Yuan Wang 5 imeidhinishwa na mamlaka ya baharini ya Sri Lanka kuweka nanga katika bandari ya Hambantota, kaskazini mwa kisiwa hiki katika Bahari ya Hindi. © youtube
Matangazo ya kibiashara

Hiki ni kipindi kipya katika vita vya ushawishi kati ya India na China nchini Sri Lanka, ambayo inakabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi katika historia yake. Meli ya Yuan Wang 5 imeidhinishwa na mamlaka ya baharini ya Sri Lanka kuegesha kwenye bandari ya Hambantota, kaskazini mwa kisiwa cha Bahari ya Hindi, ameripoti mwandishi wetu huko Bangalore, Côme Bastin.

Hata hivyo, kulingana na idara ya kijasusi ya India, meli hii inaweza kutumika kufuatilia satelaiti na kufanya ujasusi, amebaini Sathiya Moorthy, mchambuzi wa masuala ya uhusiano wa kimataifa huko Madras: "Melihii inaweza kutumika kutengeneza ramani ya mali ya kijeshi ya India Kusini: vifaa vya nyuklia, jeshi la majini. makao makuu ya jeshi la anga. Aidha, bandari ambayo iimeipa nafasi ya kuegesha meli hiyo imekodishwa kwa China. Shughuli yoyote ya kijeshi ni marufuku katika eneo hailo. Lakini hii sio mara ya kwanza kuona meli kama hizo zikiwa na uwezo wa matumizi mawili. Kwa hali hii nilazima India ipatwe na wasiwasi lakini pia Maldives, Sri Lanka au Mauritius. »

Bandari ya kina kirefu ya Hambantota ilifadhiliwa na kujengwa na benki pamoja na kampuni ya China. Mnamo mwaka wa 2017, Sri Lanka ilitoa mkataba wa miaka 99 juu ya shughuli za kibiashara za bandari hiyo kwa kampuni ya China ya China Merchants.

Meli hiyo ya kijasusi inatarajiwa kuwasili siku yaJumanne, Agosti 16. Ingawa inatambuliwa kuwa Sri Lanka ni nchi huru, diplomasia ya India imelalamikia kwa nguvu hali hiyo kwa serikali ya Colombo, bila mafanikio.

Wizara ya Mambo ya Nje imesema itafuatilia kwa karibu "athari zozote kwa usalama na maslahi ya kiuchumi ya India na kuchukua hatua zote muhimu ili kuzilinda".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.