Pata taarifa kuu

Sri Lanka: Baada ya hali ya hatari, watu wana matumaini ya kuwa na maisha mazuri

Hali ya hatari imeondolewa tangu Alhamisi asubuhi nchini Sri Lanka baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kutaka kujiuzulu kwa Rais Gotabaya Rajapaksa. Nchini, hali ya uchumi bado ni ya wasiwasi na wakazi wa nchi hiyo wanatumai kuimarika kwa gharama ya maisha.

Uhaba wa bidhaa unaathiri sekta zote za uchumi wa kisiwa cha Bahari ya Hindi, Sri Lanka.
Uhaba wa bidhaa unaathiri sekta zote za uchumi wa kisiwa cha Bahari ya Hindi, Sri Lanka. © Jelena Tomic / RFI
Matangazo ya kibiashara

Tangu katikati ya mwezi wa Julai rais mpya aliyechaguliwa na bunge ni Ranil Wickremesinghe. Alipochagua tu kuondoa hali ya dharura, maandamano madogo yalizuka huko Colombo. Wanafunzi ndio waliojitokeza na kutawanywa haraka na polisi, lakini hii inaonyesha kuwa hali bado ni tete. Tangu kuanza kwa maandamano hayo, vijana wamejitokeza kwa kiasi kikubwa katika maandamano ya vuguvugu la uasi linaloitwa Aragalaya. Maandamano hayo yalitulia taratibu baada ya kujiuzulu kwa Rajapaksa, kuundwa kwa serikali mpya, lakini pia kutawanywa kwenye eneo la kihistoria kwa waandamanaji huko Colombo ambayo Ranil Wickremesinghe aliamuru mara tu alipochukua mamlaka, ikifuatiwa na hali ya dharura.

Leo, raia wanalengwa kwa mashambulizi ya vikosi vya usalama. Ranil Wickremesinghe, hata kama hatoki chama kimoja na Rajapaksa, alikuwa Waziri Mkuu katika utawala wa rais anayechukiwa na ambaye anachukuliwa kuwa rafiki wa karibu. Lakini katika hotuba yake ya ufunguzi, aliahidi kushirikiana na vyama vyote kwa kuijenga nchi.

Wakazi nao wamechoshwa sana na mgogoro wa kiuchumi na mgogoro wa kisiasa, hivyo kwa sasa wanaonekana kumpa nafasi. Lakini vuguvugu la Aragalaya pia limevunjika na sehemu inayohitajika zaidi, hasa vijana, baada ya wengi wao kukamatwa alipochukuwa madaraka. Kwa hiyo vijana wanaweza kuanza tena maandamano wakati wowote. Itabidi kuchukua hatua kali, hasa kubatilisha marekebisho ya 20 ya katiba ambayo Rajapaksa alipitisha ili kuimarisha mamlaka ya rais. Ranil Wickremesinghe amejitolea kufanya hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.