Pata taarifa kuu
Sri Lanka-siasa

Sri Lanka: Yanafanyika mazungumzo ya kuachia majengo ya serikali yaliotekwa na raia

Waandaaji wa maandano dhidi ya utawala wa rais Rajapaksa nchini  Sri Lanka wanafanya mazungumzo yanayonuia  kurejesha majengo ya serikali walioyachukua wakati wa maandamano ya kumtaka rais na waziri mkuu  kujiuzulu.

Raia nchini Sri Lanka wakipika ndani ya makazi ya waziri mkuu baada ya kuyavamia wiki hii.
Raia nchini Sri Lanka wakipika ndani ya makazi ya waziri mkuu baada ya kuyavamia wiki hii. REUTERS - DINUKA LIYANAWATTE
Matangazo ya kibiashara

Rais Gotabaya Rajapaksa alilazimika kutorokea katika visiwa vya Maldives  wiki hii baaada ya waandamanaji kuchukua makazi yake rasimi walipowazidi nguvu walinzi wake wikendi iliyopita ambapo pia walivamia ofisi ya waziri mkuu Ranil Wickremesinghe .

Wickremesinghe , ambaye Rajapaksa alimtaja kuwa rais wa muda wakati akiwa mafichoni amewataka raia kuondoka katika majengo ya serikali akiwataka pia walinda usalama kuhakikisha wanarejesha utulivu  nchini humo.

Maelfu ya waandamanaji wamekuwa waziru makazi hayo rasimi ya rais tangu kufunguliwa kwa umma baada ya Rajapaksa kutoroka walinzi wake wakisalimu amri.

Katika hotuba yake baada ya maelfu ya waandamanji kuchukua afisi yake jijini Colombo, Wickremesinghe amesema  watu wanaoingia afisini mwake wanalengo la kumzuia kutekeleza majukumu yake kama rais wa muda.

Makataa ya watu kutembea nje usiku yaliokuwa yametangazwa na waziri mkuu, yameondolewa mapema alhamis polisi wakisema  mwanajeshi mmoja na afisa wa polisi walijeruhiwa wakati wa makabiliano ya usiku nje ya majengo ya bunge kati ya walinda usalama na waandamanaji.

Watu 85 wamelaziwa wakiwa na majeraha mtu moja akiripotiwa kufariki baada ya kuathiriwa na moshi wa gesi ya kutoa machozi iliyotupwa na polisi nje ya afisi ya waziri mkuu, imesema taarifa ya hosipitali wanakolazwa 85 hao.

Rajapaksa alikuwa ameahidi kuwa atajiuzulu siku ya jumatano japokuwa hakufanya hivyo.

Kwa sasa rais huyo yuko visiwani Maldives, ambapo anatarajiwa kuelekea nchini Singapore na mkewe Ioma pamoja na walinzi wake wawili.

Vyanzo vya kidplomasia vinasema kuwa juhudi za Rajapaksa kutafuta visa ya kumpeleka Marekani zimekataliwa kwa msingi kuwa alifuta uraia wa marekani mwaka 2019 kabla ya kuwania urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.