Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Putin: Urusi itapeleka silaha za nyuklia Belarusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Jumamosi Machi 25 kwamba Moscow itapeleka silaha za 'mbinu' za nyuklia kwenye ardhi ya mshirika wake, Belarusi, kwenye milango ya Umoja wa Ulaya, inayogawana mipaka na nchi mbili za Baltic, Poland, lakini pia, nje Umoja wa Ulaya, Ukraine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin atisia kupeleka silaha Belarusi.
Rais wa Urusi Vladimir Putin atisia kupeleka silaha Belarusi. AP - Mikhail Metzel
Matangazo ya kibiashara

"Hakuna jambo lisilo la kawaida hapa: Marekani imekuwa ikifanya hivi kwa miongo kadhaa. Kwa muda mrefu wamekuwa wakipeleka silaha zao za mbinu za nyuklia kwenye ardhi za washirika wake,” Putin amesema katika mahojiano yaliyorushwa na televisheni ya Urusi. "Tulikubali kufanya vivyo hivyo," ameongeza, akisema aliafikiana na Minsk.

Hata hivyo, ametishia kutumia makombora ya uranium yaliyopungua nchini Ukraine ikiwa Kyiv itayapokea kutoka nchi za Magharibi, kama ilivyotajwa na afisa wa Uingereza. "Urusi, kwa kweli, ina kitu cha kujibu. Tuna mamia ya maelfu ya makombora kama hayo. Hatuyatumii kwa sasa,” amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.