Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini: Jong-un ataka "kuimarisha" uwezo wake wa nyuklia

Katika kuadhimisha miaka 90 ya Jeshi la Wananchi, Korea Kaskazini imefanya gwaride kubwa la kijeshi katikati mwa mji wa Pyongyang. Utawala wa Kim Jong-un umeweza kuonyesha makombora na mizinga yake kwa raia wake, lakini hotuba ya kiongozi wa Korea Kaskazini ndio iliyowavutia sana watazamaji.

Magari yaliyobeba makombora wakati wa gwaride la kijeshi, Aprili 24, 2022.
Magari yaliyobeba makombora wakati wa gwaride la kijeshi, Aprili 24, 2022. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Vifaru, makombora, askari wa miamvuli waloanguka kutoka kwenye umbali wa juu wa zaidi ya kilomita 4,000 na fataki zilifyatuliwa katika uwanja wa Kim Il-Sung kufunga mwezi wa Aprili ambao ni muhimu kwa siku za maadhimisho ya kuanzishwa kwa baadhi ya matukio. Huko Pyongyang, miaka 110 ya mwanzilishi wa utawala na miaka 90 ya jeshi la wananchi iliadhimishwa mwezi huu, ameripoti mwandishi wetu wa Seoul, Nicolas Rocca.

Fursa kwa Kim Jong-un kusisitiza juu ya nia yake ya kubadilisha na kuboresha zilaha zake za nyuklia. "Tutaendelea kuchukua hatua za kuimarisha na kuendeleza uwezo wa nyuklia wa taifa letu kwa kasi kubwa," amesema Kim Jong-un, ambaye matamshi yake yaliripotiwa na shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA.

"Silaha za nyuklia, ishara ya nguvu zetu za kitaifa na katikati ya nguvu zetu za kijeshi, lazima ziimarishwe kwa ubora zaidi," ameongeza.

"Adui Mkuu"

Kulingana na Go Myung-hyun, mtafiti katika Taasisi ya Asan huko Seoul, "Kim Jong-un am'elezea kuwa uwezo wa nyuklia wa Korea Kaskazini sio tu hauna tu jukumu la kuzuia, lakini pia unafanya kazi nyingine." "Ilikuwa wazi kwamba alikuwa akisisitiza kwamba Korea Kaskazini inatumia silaha za nyuklia kulinda maslahi yake ya kitaifa. Unaweza kufafanua maslahi ya taifa kwa njia nyingi, lakini nadhani alikuwa akimaanisha matumizi ya silaha za nyuklia kwa madhumuni fulani,” amesema.

Makombora kadhaa yaliyofichuliwa bado hayajajaribiwa na serikali na huenda yakajaribiwa hivi karibuni. Labda kabla ya Mei 10, tarehe ya kuapishwa kwa Yoon Seok-yeol, rais mpya wa Korea Kusini ambaye alikuwa ameiita Korea Kaskazini "adui mkuu wa nchi yake".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.