Pata taarifa kuu

Makombora kadhaa yarushwa kutoka Korea Kaskazini

"Korea Kaskazini imefanya kile kinachoonekana kuwa urushwaji wa roketi nyingi asubuhi ya leo. Jeshi letu lilikuwa likifuatilia hali hiyo na likasimama tayari kuingilia kati,” imesema makao makuu ya jeshi nchini Korea Kusini katika taarifa, bila kutoa maelezo zaidi, shirika la habari la Reuters limeripoti.

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kaskazini imefanya majaribio ya urushaji makombora.
Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kaskazini imefanya majaribio ya urushaji makombora. REUTERS - KIM HONG-JI
Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap limeripoti kuwa Korea Kaskazini imerusha roketi kwenye pwani yake ya magharibi.

Baraza la Usalama la Kitaifa la Korea Kusini limefanya mkutano wa dharura kuhusiana na uzinduzi huo. Korea Kaskazini imezindua aina kadhaa mpya za mifumo mingi ya mitambo ya kurusha roketi katika miaka ya hivi karibuni, na kuongeza kwa safu kubwa ya silaha ambazo zinaweza kulenga maeneo yanayowezekana Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.