Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-SIASA

Korea Kaskazini yaendelea kutawaliwa chini ya Familia ya Kim

Korea Kusini imeadhimisha miaka 10 tangu kufariki dunia kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Il, huku maelfu wakijitokeza akiwemo mwanaye ambaye ndio kiongozi wa sasa Kim Jong Un.

Kim Jong Unkiongozi wa Korea Kaskazini.
Kim Jong Unkiongozi wa Korea Kaskazini. STR KCNA VIA KNS/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Katika maadhimosho hayo, Kim Jong Un alionekana akiinamia na kutoa heshima mbele ya picha kubwa ya baba yake jijini Pyongyang, huku bendera zikipepea nusu mlingoti. Watu waliofika katika maadhimisho hayo pia waliinamisha vichwa vyao kama ishara ya kutoa heshima.

Kim Jong Il aliongoza Korea Kaskazini kwa miaka 17 hadi alipofariki dunia Desemba mwaka 2011 na mtoto wake wa kiume Kim Jong Un akachukua madaraka.

Vizazi vitatu vya Familia ya Kim, vimeongoza nchi hiyo tangu mwaka 1948 na raia wanaozaliwa nchini humo wanafunzwa kuwaenzi Kim Il Sung na Kim Jong Il na watu wazima  nchini humo huvalia kitambulisho kinachowatambulisha viongozi hao wa zamani.

Chini ya uongozi wa familia ya Kim, nchi hiyo imefanIkiwa kupata silaha za maangamizi za masafa marefu lakini pia zile za nyuklia na kutishia usalama wa nchi jirani, lakini uchumi wa nchi hiyo Umeendelea kushuka huku wananchi wakishuhudia uhaba wa chakula.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.