Pata taarifa kuu

Tokyo na Seoul zakumbwa na mzozo kuhusu migodi ya dhahabu ya Kisiwa cha Sado

Kwa wiki kadhaa, Korea Kusini na Japan zimekuwa katika mzozo wa kidiplomasia kuhusu suala la migodi ya dhahabu katika kisiwa cha Sado.

Picha iliyotolewa na Walinzi wa Pwani ya Japani kwenye Kisiwa cha Sado.
Picha iliyotolewa na Walinzi wa Pwani ya Japani kwenye Kisiwa cha Sado. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Tokyo imezindua kampeni ya migodi yake kutambuliwa kama eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO. Lakini Seoul imekasirishwa, kwa sababu eneo hili lilitumiwa kwa kazi za kulazimishwa kwa wakazi wa Korea wakati wa askari wa Japan walipokuwa wakikalia eneo hilo kimabavu. Mzozo wa kihistoria ambao unaendelea kudidimiza uhusiano ambao tayari umeyumba.

"Japani inapuuzia historia mbaya ya kazi za kulazimishwa zinazodaiwa na Korea. Shutuma za Seoul zinajumlisha pengo kubwa la mitazamo inayotenganisha miji mikuu miwili.

Ikiwa migodi ya dhahabu na fedha ya Sado, iliyotumiwa tangu karne ya 17, ni ishara ya ukuaji wa viwanda nchini Japani, pia ilikuwa eneo la kazi ya kulazimishwa wakati wa ukoloni wa Korea kati ya mwaka 1910 na 1945.

Wakorea wapatao 780,000 walishiriki kwa hiari au kwa nguvu katika maendeleo ya viwanda vya Japani, wakiwemo 2,000 katika migodi ya Sado, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia pekee.

Na ndiyo maana uamuzi wa Japani unaiudhi Seoul, kwa sababu Tokyo haitaji waathiriwa wa kazi ya kulazimishwa katika maombi yake kwa UNESCO. Tayari katika mwaka wa 2015, karibu maeneo ishirini ya viwanda ambapo matukio kama hayo yalifanyika yalikuwa yameorodheshwa kama Urithi wa Dunia.

Marekani kwa upande wake inawataka washirika wake kutatua haraka tofauti zao ili kuzingatia vitisho vinavyotolewa na China na Korea Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.