Pata taarifa kuu
JAPANI-USHIRIKIANO

Japan yaongeza mchango wa kifedha kwa vikosi vya Marekani

Japan, Ijumaa wiki hii imetangaza mchango wake wa kifedha kwa vikosi vya Marekani kwenye vilioko nchini humo, dhidi ya hali ya kuongezeka kwa mvutano wa kikanda kati ya China na Korea Kaskazini, lakini pia msuguano kati ya Tokyo na Washington juu ya mgogoro wa kiafya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Japan Yoshimasa Hayashi na Nobuo Kishi katika mkutano kwa njia ya video, Januari 6, 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Japan Yoshimasa Hayashi na Nobuo Kishi katika mkutano kwa njia ya video, Januari 6, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huu mpya wa miaka mitano uliotiwa saini Ijumaa, Januari 7 utawezesha "kuwekeza rasilimali zaidi ili kuimarisha upatikanaji wetu wa kijeshi na ushirikiano," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kilele wa mtandao kati ya mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa nchi hizi mbili.

Mchango mpya wa Japan unafikia yen bilioni 211 kwa mwaka, au yen bilioni 1,055 kwa jumla (sawa na euro bilioni 8), kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japani iliyohojiwa na shirika la habari la AFP. Hii ni sawa na ongezeko la karibu 5% ikilinganishwa na kipindi cha awali.

Kwa mujibu wa mkataba wa usalama kati ya Japani na Marekani ulioanza mwaka wa 1960, Washington inahakikisha ulinzi wa kijeshi wa Japani, ambayo ina "vikosi vya kujilinda" tu kwa uwezo na kazi zilizowekewa kikomo. Lakini Tokyo imelazimika kutoa gharama zinazohusiana na kuwepo kwa baadhi ya askari 50,000 wa Marekani waliowekwa kwenye ardhi yake.

"Vitendo vya Uchochezi vya China", "Tishio la Kudumu" kutoka Korea Kaskazini

Antony Blinken alikumbusha leo Ijumaa "vitendo vya uchochezi vya Beijing vinavyoongeza mvutano katika Mlango wa Bahari wa Taiwan, na vile vile katika bahari ya China mashariki na Kusini". Pia ameelezea programu za Korea Kaskazini kama "tishio linaloendelea," Pyongyang wiki hii ilidai kuwa ilifanya majaribio ya kurusha kombora la hypersonic.

Katika taarifa ya pamoja, mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Marekani na Japan leo Ijumaa pia wameeleza "wasiwasi wao wa kina na wa kudumu" kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu katika mkoa wa Xinjiang wa China na Hong Kong, na kutoa wito wa "amani na utulivu" katika Mlango wa Taiwan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.