Pata taarifa kuu
BURMA-USALAMA

Burma: Mapigano yaongezeka katika jimbo la Kayah, Thailand yatuma kikosi cha msaada

Huku nchi mbalimbali zikiendelea kulaani shambulio la Desemba 24 dhidi ya raia lililosababisha vifo vya watu 35 katika jimbo la Kayah nchini Burma, mapigano yanazidi kuwa makali katika eneo linalopakana na Thailand, na kusababisha wimbi la maelfu ya wakimbizi. Jeshi la Thailand linatuma vikosi zaidi kulinda eneo hilo.

Ijumaa, Desemba 24, shambulio katika kijiji kimoja lilisababisha vifo vya raia 35.
Ijumaa, Desemba 24, shambulio katika kijiji kimoja lilisababisha vifo vya raia 35. © AP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano ya ardhini, urushaji wa mabomu, magari kuchomwa moto, hiyo ndio hali inayoshuhudiwa katika uwanja wa mapigano nchini Burma ... Sasa ni vita vya wazi kati ya jeshi la Burma, Tatmadaw na wanamgambo kadhaa wenye silaha, hasa Muungano wa Kitaifa wa Karen, moja ya vikosi vya zamani zaidi vya kikabila na vikosi vya Ulinzi vya Karen. Raia, kundi jipya lililoundwa hivi karibuni, ambalo limejumuisha raia wenye silaha kutoka maeneombalimbali ya nchi hiyo.

 

Wanajeshi hao wa Burma pia wanatuhumiwa kufanya msako katika vijiji ili kuadhibu mshikamano wowote na wapiganaji. Wakati mapigano yamedumu kwa miezi kadhaa, kurejea kwa msimu wa kiangazi katika wiki za hivi karibuni kumewezesha kufikia maeneo makubwa ya mapigano.

Wanakijiji wanakimbilia Thailand

Maelfu ya wanakijiji wamekimbilia nchi jirani ya Thailand. Zaidi ya 5,000 kati yao wameruhusiwa kubaki katika ardhi ya Thailand kwa misingi ya kibinadamu. Ishara isiyo ya kawaida inayoonyesha uzito wa hali hiyo.

Jeshi limetangaza kwamba linaongeza uwepo wake katika mkoa wa mpaka wa Tak, huku wanakijiji wanaoishi karibu sana na mstari wa mbele wa vita wanaweza kuhamia kwenye mahekalu na mabohari.

Umoja wa Mataifa unatoa wito wa uchunguzi "kamili na wa uwazi" kuwafikisha waliohusika mbele ya sheria baada ya shambulio lililosababisha vifo vya watu 35 katika kijiji kimoja katika jimbo la Kayah. Mjumbe Maalumu mpya wa Umoja wa Mataifa kwa Burma Noeleen Heyzer amesema "ana wasiwasi mkubwa" kuhusu kuongezeka kwa ghasia nchini humo na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano wakati dunia ikisheherekea Mwaka Mpya.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi zinaonyesha magari kadhaa yamechomwa moto karibu na kijiji cha Moso, kunakoishi watu kutoka jumuiya ya Wakristo, katika kitongoji cha Hpruso, mashariki mwa jimbo la Kayah. Katika kijiji hiki, kwa uchache watu 35 - ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto - waliuawa na kuchomwa moto na jeshi, kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali

Jeshi hilo lilisema katika taarifa yake siku ya Ijumaa kwamba magari yaliyopatikana katika eneo la tukio hayakusimama kwa ajili ya ukaguzi kama ilivyoamriwa na kwamba baadhi ya "magaidi" katika kundi hilo walianza kuwafyatulia risasi askari hao ambao walilipiza kisasi. Lakini taarifa kwa vyombo vya habari haijataja magari au miili iliyoungua.

Shirika la misaada ya kibinadamu la Save the Children limesema wafanyakazi wake wawili waliokuwa wakirejea ofisini baada ya kutekeleza shughuli za usaidizi katika jamii iliyo karibu, walikwama kutokana na tukio hilo na bado hawajulikani walipo. Shirika hilo lisilo la kiserikali linasema limepata uthibitisho kwamba gari lao la kibinafsi lilivamiwa na kuchomwa moto. Wanajeshi hao wanaripotiwa kuwalazimisha watu kutoka kwenye magari yao, kuwakamata baadhi, kuwaua wengine na kuchoma miili yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.