Pata taarifa kuu
URUSI-USHIRIKIANO

Urusi yapokea ujumbe wa Taliban kujadili utulivu nchini Afghanistan

Urusi inapokea Jumatano hii, Oktoba 20 huko Moscow ujumbe wa serikali mpya ya Kabul. Taliban wamewekwa kwenye orodha "magaidi" tangu miaka ya 2000, lakini njia za majazungumzo na Moscow zimekuwa wazi kila wakati. Na Urusi ina lengo moja kuu: utulivu upande wake wa kusini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Sochi, usiku wa kuamkia mazungumzo kuhusu Afghanistan nchini Urusi. Marekani ilitangaza Jumatatu, Oktoba 18 kwamba haitashiriki katika mkutano huo ambao utahudhuriwa na Urusi, China na Pakistan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Sochi, usiku wa kuamkia mazungumzo kuhusu Afghanistan nchini Urusi. Marekani ilitangaza Jumatatu, Oktoba 18 kwamba haitashiriki katika mkutano huo ambao utahudhuriwa na Urusi, China na Pakistan. via REUTERS - Russian Foreign Ministry
Matangazo ya kibiashara

Oktoba 3, 2021: mlipuko katika msikiti huko Kabul uliua karibu watu 20 na kujeruhi zaidi ya wengine 30. Urusi ni moja ya nchi za kwanza kabisa kutoa taarifa kulaani shambulio hilo lililodaiwa kutekelezwa na na kundi la Islamic State.

Oktoba 15: Vladimir Putin alisema ana wasiwasi kuhusu nguvu na malengo ya kundi hili la wanajihadi. Wapiganaji 2,000 wanajiandaa kupanua ushawishi wao katika ukanda wa Asia ya Kati na katika maeneombalimbali nchini Urusi, alisema rais Putin. Miongoni mwao ni wanajihadi waliopewa mazoezi makubwa ya kijeshi kutoka Syria na Iraq, rais wa Urusi alibaini mapema wiki hii.

Wakati huo huo Urusi imesitisha ujumbe wake katika Jumuiya ya Kujihami ya NATO na kuamuru kufungwa kwa ofisi zake mjini Moscow. Hatua hiyo ni ya ulipizaji kisasi baada ya NATO kuwatimua wanadiplomasia wanane wa Moscow mapema mwezi huu, ikidai kuwa walikuwa wakifanya kazi kama majasusi.

Hata hivyo, Urusi imetupilia mbali madai hayo kuwa hayana misingi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema mawasiliano yoyote baina ya pande hizo mbili yatapitia katika ubalozi wa Urusi nchini Ubelgiji.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas amekosoa uamuzi huo uliochukuliwa na Moscow, akisema utazidisha hali ngumu ambayo imekuwepo na kutia doa zaidi mahusiano ya pande hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.