Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Makumi ya watu wauawa baada ya milipuko katika msikiti wa Kandahar

Milipuko hiyo ilitokea wakati wa sala kuu ya Ijumaa kwenye msikiti wa Washia katika mji wa Kandahar, kusini mwa Afghanistan. Mtu wa kujitoa mhanga alijilipua, kulingana na afisa wa Taliban, shambulio ambalo linakuja wiki moja baada ya shambulio jingine dhidi ya msikiti wa Washia kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, huko Kunduz, ambalo liligharimu maisha ya watu kadhaa.

Vikosi vya Taliban vikitoa ulinzia karibu na msikiti wa Kishia huko Kandahar ambapo milipuko kadhaa ilisababisha watu kadhaa kupoteza maisha Ijumaa, Oktoba 15, 2021.
Vikosi vya Taliban vikitoa ulinzia karibu na msikiti wa Kishia huko Kandahar ambapo milipuko kadhaa ilisababisha watu kadhaa kupoteza maisha Ijumaa, Oktoba 15, 2021. © AFP - JAVED TANVEER
Matangazo ya kibiashara

Picha kwa sasa haziwezekani kuthibitisha. Lakini zile zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha miili iliyojaa damu ikiwa imelala chini ndani ya Msikiti wa Fatemieh, pia unaojulikana kama Msikiti wa Imam-Bargah.

Kulingana na chanzo cha hospitali, watu wasiopungua 33 wameuawa na 74 wamejeruhiwa katika mlipuko mmoja au zaidi uliotokea Ijumaa adhuhuri katika msikiti huu wa Kishia katika mji wa Kandahar, kusini mwa Afghanistan. Mlipuko huo ulitokea mahali pa ibada ya Washia, katikati mwa Kandahar, wakati wa sala ya Ijumaa ya kila wiki.

Mmoja wa mashuhuda amesema waripuaji wanne wa kujitoa muhanga waliushambulia msikiti huo. Wawili wakaripua mabomu yao katika lango la usalama, hivyo kuwawezesha wawili wengine kukimbilia ndani na kuushambulia umati wa waumini

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.