Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Mazungumzo ya kwanza kati ya Wamarekani na Taliban tangu kuanguka kwa Kabul

Jumapili hii Oktoba 10, ni siku ya pili ya mazungumzo huko Doha nchini Qatar kati ya ujumbe kutoka Marekani na Taliban. Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika tangu Marekani ilipojiondoa nchini Afghanistan.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Kabul mnamo Agosti 31, 2021.
Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Kabul mnamo Agosti 31, 2021. AFP - WAKIL KOHSAR
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yalianza siku moja baada ya shambulio la bomu la kujitoa mhanga lililodaiwa na kundi la Islamic State dhidi ya msikiti huko Kunduz, na kuua watu wasiopungua 60. Makubaliano ya Doha ya Februari 2020 pamoja na misaada ya kibinadamu, kati ya mambo mengine, yako katika ajenda ya mazungumo hayo.

Kwa upande wa Marekani, inasema mazungumzo haya yana malengo manne, kulingana na taarifa za hivi karibuni za baadhi ya maafisa wa Marekani. Kwanza, kuhamasisha Taliban kuunda serikali ya umoja.

Hoja nyingine ambayo ujumbe wa Marekani unataka kusisitiza: kuheshimu haki za Waafghan, hasa haki za wasichana na wanawake. Wanawake bado hawaruhusiwi kufanya kazi katika ofisi pamoja na wanaume au serikalini.

Washington pia inatarajia kuwashawishi Wataliban kuruhusu mashirika ya misaada kufika katika maeneo yenye shida wakati nchi hii inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.