Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-HAKI

Mwendesha Mashtaka wa ICC ataka uchunguzi nchini Afghanistan uendelee

Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC Karim Khan ameomba kupatiwa idhini ya kuendelea na uchunguzi juu ya makosa ya kivita nchini Afghanistan akisema watawala wapya nchini humo hawawezi kusimamia kwa ufanisi uchunguzi wa ndani.

Kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi yake Khan amesema sasa analenga kuweka umuhimu katika kuchunguza makosa yaliyofanywa na kundi la Taliban na washirika wake badala ya masuala mengine ikiwemo matendo yaliyofanywa na vikosi vya Marekani.
Kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi yake Khan amesema sasa analenga kuweka umuhimu katika kuchunguza makosa yaliyofanywa na kundi la Taliban na washirika wake badala ya masuala mengine ikiwemo matendo yaliyofanywa na vikosi vya Marekani. WAKIL KOHSAR AFP
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa ICC waliidhinisha uchunguzi uliopendekezwa na mtanguliizi wa Khan, Fatou Bensouda uliolenga kuchunguza makosa yaliyofanywa na vikosi vya Afghanistan, kundi la Taliban na taasisi za kijasusi za Marekani yaliyofanywa tangu mwaka 2002.

Kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi yake Khan amesema sasa analenga kuweka umuhimu katika kuchunguza makosa yaliyofanywa na kundi la Taliban na washirika wake badala ya masuala mengine ikiwemo matendo yaliyofanywa na vikosi vya Marekani.

Hatua ya kuchunguza makosa ya Wamarekani iliikasirisha serikali mjini Washington na kutangaza vikwazo dhidi ya Bensouda kabla ya baadaye kuamuliwa uchunguzi huo ufanywe na mamlaka za ndani nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.