Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Taliban yatangaza sehemu ya serikali yake mpya

Taliban imetangaza majina ya kwanza yaliyosubiriwa kwa muda mrefu ya serikali mpya.  Mohammad Hassan Akhund ameteuliwa kuwa kiongozi wa serikali mpya, wiki tatu baada ya Taliban kuchukua madaraka nchini Afghanistan.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid ametangaza majina ya kwanza ya serikali mpya ya Taliban Jumanne jioni, Septemba 8, 2021. Hapa ni katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari huko Kabul, Afghanistan Agosti 17, 2021.
Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid ametangaza majina ya kwanza ya serikali mpya ya Taliban Jumanne jioni, Septemba 8, 2021. Hapa ni katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari huko Kabul, Afghanistan Agosti 17, 2021. AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

Taliban imetangaza sehemu ya serikali yake mpya ambayo itaongozwa na Mohammad Hassan Akhund. Mwanzilishi mwenza wa Taliban Abdul Ghani Baradar ameteuliwa kuwa naibu kiongozi wa serikali mpya, msemaji mkuu wa Taliban ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari huko Kabul Jumanne hii jioni.

Abdul Ghani Baradar, ambaye anaheshimiwa na kusikilizwa na makundi mbalimbali, aliongoza mazungumzo ya Doha na kati ya Taliban na Marekani, ambayo yaliwezesha kuondolewa kwa vikosi vya kigeni nchini Afghanistan.

Mullah Yaqoub, mtoto wa Mullah Omar, ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi, na Sirajuddin Haqqani, mkuu wa mtandao wa Haqqani ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani. Sirajuddin Haqqani anaongoza tawi la kijeshi la Taliban, mtandao wa kigaidi. Mtandao wa Haqqani ndio uliohusika na mashambulio yaliyotekelezwa kwa kipini cha miaka 20 iliyopita dhidi ya vikosi vya kigeni, vikosi vya serikali ya Afghanistan na raia.

Amir Khan Muttaqi, mshauri wa Taliban huko Doha, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

"Serikali haijakamilika," alisema msemaji Zabihullah Mujahid, akihakikishia kwamba Taliban, ambayo iliahidi kuwashirikisha watu mbalimbali katikaserikalihiyo mpya, itajaribu "kuchukua watu kutoka mikoa mingine ya nchi".

Taliban imerejea madarakani miaka ishirini baada ya kuondolewa mamlakani na muungano ulioongozwa na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.