Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani ziarani Doha kuijadili Kabul

Afghanistan itakuwa katika agenda ya mazungumzo katika kikao cha viongozi huko Doha, nchini Qatar, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatarajia kuwasili leo Jumatatu Septemba 6, Kisha ataendelea na ziara yake hadi nchini Ujerumani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Agosti 2021 huko Washington.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Agosti 2021 huko Washington. AP - Olivier Douliery
Matangazo ya kibiashara

Ni ziara ya kuzishukuru nchi zinazowapa hifadhi Waafghan waliohamishwa na Marekani na washirika wao kutoka uwanja wa ndege wa Kabul mwishoni mwa mwezi Agosti.

Anthony Blinken anatarajiwa kukutana na Emir Tamim bin Hamad Al Thani, pamoja na Waziri wa Mambo ya nje. Waziri wa Mambo ya Nje wa Maekani anatarajiwa kuzuru moja ya vituo vya kupokea wakimbizi.

Baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, wanadiplomasia wa Marekani walihamishwa karika mji mkuu wa Qatar, Doha, ili kushughulikia mambo ya kibalozi na kidiplomasia kwa Afghanistan.

Wakati Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inahakikisha kuwa njia za mawasiliano bado ziko wazi na Taliban, haijulikani ikiwa Antony Blinken atakutana na maafisa wa Taliban huko Qatar.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani atasafiri kwenda nchini Ujerumani, ambapo atazuru kituo cha Ramstein, ambacho pia kilitumiwa katika shughuli za uokoaji. Atashiriki pia katika mkutano uliopangwa kujadili hali ya Afghanistan, na nchi zingine ishirini zitashiriki katika mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.