Pata taarifa kuu
PAKISTANI-USALAMA

Afghanistan: Mkuu wa idara ya ujasusi wa jeshi la Pakistani ziarani Kabul

Mapigano yanaendelea katika bonde la Panshir, ngome ya mwisho ya upinzani dhidi ya watu wenye msimamo mkali wa kidini kutoka kundi la Taliban. Taliban bado hawajatangaza serikali yao.

Askari wa Taliban kwenye moja ya barabara huko Kabul, Septemba 4, 2021.
Askari wa Taliban kwenye moja ya barabara huko Kabul, Septemba 4, 2021. AP - Wali Sabawoon
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni walitoa wito kwa balozi za kigeni kurejea nchini. Jumamosi hii, Septemba 4, mkuu wa idara ya ujasusi wa jeshi la Pakistani Faiz Hameed alizuru Kabul. Alitarajia kukutana kwa mazungumzo na maafisa wakuu wa Taliban.

Hakuna taarifa yoyote kuhusiana na ziara hii au juu ya yaliyomo kwenye mazungumzo kati ya Faiz Hameed na wawakilishi wa Taliban aliyetarajia kukutana nao. Ziara hii jijini Kabul, hata hivyo, inathibitisha uhusiano kati ya Taliban kutoka Afghanistan na Pakistan, kwa sababu mbali na wawakilishi wa Qatar, nchi chache sasa zinajionyesha kuunga mkono Taliban, washindi wa vita virefu zaidi katika historia ya Marekani.

Tangu Taliban kuchukua madaraka, serikali ya Pakistan imetoa wito wa kuundwa kwa "serikali ya umoja", ambayo itajumuisha wajumbe kutoka makabila yote." Islamabad pia inatoa wito kwa muundo wa serikali ambao haki za msingi za raia wote zitalindwa.

Muungano Dhidi ya Taliban kutoka Pakistan

Pakistan ina uhusiano wa kipekee na Taliban ambayo imewakilishwa na pande mbili huko kwa miaka mingi: Shura ya Quetta na ile ya Peshawar. Kwa upande wa usalama, Pakistan ina nia kubwa ya kuendelea kudumisha uhusiano mzuri na jirani yake.

Mpaka kati ya nchi hizi mbili sasa umewekwa uzio. Hata hivyo, haizuii mtu yoyoe kuvuka kwenda upande wa pili. Mamlaka ya Pakistan ambayo inapigana na makundi kadhaa ya kigaidi kwenye ardhi yake, kama vile TTP, Taliban kutoka Pakistan, pia inataka kuhakikisha kuwa Kabul itakuwa mshirika wake katika vita hivi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.