Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Mapigano yanapamba moto Panshir

Taliban imeahirisha kutangaza serikali mpya, ambayo muundo wake unaweza kuzua sintofahamu kwa miaka ijayo nchini Afghanistan. Utawala mpya bado unakabiliwa na upinzani mkubwa wa kijeshi katika bonde la Panshir.

Wapiganaji wa kundi linalopambana na Taliban katika wilaya ya Dara, katika jimbo la Panshir, Afghanistan, Septemba 2, 2021.
Wapiganaji wa kundi linalopambana na Taliban katika wilaya ya Dara, katika jimbo la Panshir, Afghanistan, Septemba 2, 2021. AFP - AHMAD SAHEL ARMAN
Matangazo ya kibiashara

Hakuna tangazo lililotolewa kuhusu serikali mpya ya Afghanistan Jumamosi hii, kulingana na vyanzo viwili vya Taliban vilivyonukuliwa na shirika la habarilaAFP. Hali katika jimbo la Panshir, moja ya ngome za mwisho za upinzani wenye silaha kwa serikali mpya, inaweza kuwa sababu ya kucheleweshwa kwa kutangazwa serikali mpya, ambayo mwanzoni ilitarajiwa kutangazwa siku ya Ijumaa.

Ngome ya muda mrefu dhidi ya Taliban, bonde hili lililozungukwa na milima na ambalo ni si rahisi kulidhibiti, liko karibu kilomita 80 kaskazini mwa mji mkuu, linakumbwa tangu Jumatatu na baaba ya kuondoka kwa askari wa mwisho wa Marekani nchini Afghanistan na mapigano kati ya vikosi vya Taliban na kundi la upinzani lenye silaha la FNR.

Siku ya Ijumaa jioni, mizinga ilisikika katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul,  kusherehekea ushindi wa Taliban huko Panshir, baada ya uvumi kwenye mitandao ya kijamii kubaini hivyo. Lakini Taliban haikutangaza rasmi na mkazi mmoja wa Panshir ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kwamba taarifa hizo ni za uwongo.

"Upinzani unaendelea"

Kulingana na idara ya huduma za dharura katika mji mkuu Kabul, watu wawili waliuawa na wengine 20 walijeruhiwa katika urushwaji risasi na hivyo kumpelekea msemaji mkuu wa Taliban, Zabihullah Mujahid, kuwasihi wafuasi wake kwenye Twitter waache "kurusha risasi hewani" na "alimshukuru Mungu ”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.