Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Qatar yataka Taliban kufungua uwanja wa ndege wa Kabul

Qatar inasema inawasiliana na viongozi wa Taliban nchini Afganistan, ili kuufungua tena uwanja wa Kimataifa wa Kabul, haraka iwezekanavyo.

Vikosi vya Taliban vikifanya doria katika moja ya mitaa ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
Vikosi vya Taliban vikifanya doria katika moja ya mitaa ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. AFP - HOSHANG HASHIMI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, anasema wanashirikiana pia na Uturuki kufanikisha mpango huo.

Nayo Uingereza kupitia Waziri wake wa Mambo ya nje Dominic Raab akiwa jijini Doha amesema, London haina mpango wa kuitambua serikali ya Taliban hivi karibuni.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa unaonya kuwa, kuna hatari ya raia wa Afganistan kukabiliwa na baa la njaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.