Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Ifahamu historia ya Taliban, Taliban ni akina nani?

Jina lao linatokana na neno "talib" ambalo linamaanisha "mwanafunzi". Ni katika shule za Korani (madrasat) za Pakistani ambapo Waafghan wa kabila la Pashtun waliunda kundi hili lenye misingi ya kisiasa na kidini.

Wapiganaji wa Taliban wakipiga doria huko Kabul, Afghanistan, Jumamosi, Agosti 28, 2021.
Wapiganaji wa Taliban wakipiga doria huko Kabul, Afghanistan, Jumamosi, Agosti 28, 2021. AP - Khwaja Tawfiq Sediqi
Matangazo ya kibiashara

Taliban ilichukua madaraka kwa mara ya kwanza mnamo 1996. Nchi hiyo ikawa makazi ya wanajihadi ambapo Al-Qaeda iliandaa mashambulio ya Septemba 11, 2001 nchini Marekani. Uvamizi wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan uliwatimua Taliban madarakani lakini Marekani haikuweza kufanikiwa kuzima uasi wa kundi hilo, na ukurasa huu wa miaka ishirini umezimwa sasa na kuondoka kwa nchi za Magharibi nchini Afghanistan.

Taliban ambao wanashinda leo wanaongozwa na Mullah Hibatullah Akhundzada ambaye Taliban wanasema ataonekana hadharani hivi karibuni. Katika siku za hivi karibuni, mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo, Mullah Baradar,  alirejea nchini.

Taliban wa mwaka 2021 wanasema wamebadilika. Walifanya mazungumzo na kufikia mkataba na Washington; wanahakikisha kuwa usimamizi wa utawala hautakuwa wa kikatili ikilinganishwa na miaka ya 90; wanaendeleza au kukuza uhusiano na Pakistan, Qatar, Iran, China na hata Urusi. Na sasa wanakabiliwa na changamoto ya kulijenga tena tafa la Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.