Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: EU kuendelea kuwepo Kabul "ikiwa hali ya usalama itaruhusu"

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamekutana nchini Slovenia kujadili mzozo wa Afghanistan Ijumaa (Septemba 3). Bila kuitambua rasmi serikali ya Taliban, Umoja wa Ulaya unasema utaanzisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ... kulingana na hali ya usalama itakavyokuwa, kuheshimu haki za binadamu na za wanawake, na pia utawala sheria.

Mmoja wa waasisi wa kundi la Taliban, Mullah Baradar (katikati), anatazamiwa wakati wowote kuanzia sasa kutangazwa kuwa kiongozi mpya wa serikali ya Afghanistan, kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika ndani ya kundi hilo
Mmoja wa waasisi wa kundi la Taliban, Mullah Baradar (katikati), anatazamiwa wakati wowote kuanzia sasa kutangazwa kuwa kiongozi mpya wa serikali ya Afghanistan, kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika ndani ya kundi hilo AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya unabaini kwamba, hali nchini Afghanistan inagubikwa na maswali juu ya usalama wa Umoja huo (EU), hatari ya mzozo wa wahamiaji na ahadi ya Ulaya ya kusaidia Waafghan ambao wanataka kuondoka nchini, na pia wale wanaotaka kubaki nchini humo.

Sababu hizi zinahitaji ushiriki "ulioratibiwa" nchini Afghanistan, kulingana na Mkuu wa sera za mambo ya nchi za nje wa umoja huo. Lakini hii "haimaanishi kutambuliwa" kwa utawala wa Taliban, ameonya

Waziri wa Mambo ya nje wa Slovenia Anze Logar (mbele-kushoto) na Mkuu wa sera za mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell waanzisha mkutano wa EU katika Jumba la Brdo Castle, Slovenia.
Waziri wa Mambo ya nje wa Slovenia Anze Logar (mbele-kushoto) na Mkuu wa sera za mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell waanzisha mkutano wa EU katika Jumba la Brdo Castle, Slovenia. Jure Makovec AFP

.

Kiwango cha ushiriki wa nchi za Umoja wa Ulaya kitategemea mwenendo wa Taliban kuhusiana na masuala matano ambayo yana vigezo vingi. Taliban kwanza itajiepusha kutotumia Afghanistan kama hifadhi kwa magaidi au nchi  inayotumika kwa kusaidia ugaidi wa kimataifa. Halafu, witalazimika kuheshimu haki za binadamu na hasa haki za wanawake, na pia sheria na uhuru wa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.