Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Taliban wadai kudhibiti jimbo la Panjshir

Jimbo la  Panjshir, lilikuwa eneo la mwisho linalokaliwa na upinzani dhidi ya Taliban tangu wapiganaji hao Kiislamu walipochukua madaraka nchini Afghanistan katikati ya mezi wa Agosti.

Vikosi vya upinzani dhidi ya Taliban katika jimbo la Panjshir.
Vikosi vya upinzani dhidi ya Taliban katika jimbo la Panjshir. Ahmad SAHEL ARMAN AFP
Matangazo ya kibiashara

Leo Jumatatu Taliban imetangaza kwamba wamechukua udhibiti kamili wa "bonde la Panjshir, ambalolilikuwa mikononi mwa upinzani tangu kuchukua madaraka nchini Afghanistan katikati ya mwezi wa Agosti. "Kwa ushindi huu, nchi yetu sasa imeondokana kabisa na vita," msemaji mkuu wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema katika taarifa.

Upinzani dhidi ya Taliban katika bonde la Panjshir (mashariki), ngome pekee ya upinzani wenye silaha dhidi ya utawala mpya wa Afghanistan, ulitoa wito kwa taarifa, wa kusitisha mapigano baada ya ripoti kuwa upinzani huo ulipata hasara kubwa mwishoni mwa wiki hii. Chama cha National Resistance Front (FNR) kimethibitisha usiku wa Jumapili 5 kuamkia Jumatatu tarehe 6 Septemba kuwa "wametoa pendekezo kwa Taliban kusitisha operesehini zao za kijeshi huko Panjshir ... na kuondoa vikosi vyao. Kwa upande wetu, tutawataka askari wetu wajiepushe na hatua yoyote ya kijeshi. " Siku ya Jumapili FNR iliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba msemaji wake Fahim Dashty, mwandishi wa habari maarufu nchini Afghanistan, na Jenerali Abdul Wudod Zara wameuawa katika mapigano ya hivi karibuni.

Panjshir ni ngome ya muda mrefu ya upinzani dhidi ya Taliban, eneo ambalo kamanda mashuhuri Ahmed Shah Massoud alisaidia kujulikana mwishoni mwa miaka ya 1990 kabla ya kuuawa na Al Qaeda mnamo 2001. FNR inaongozwa na Ahmad Massoud, mtoto wa Kamanda Massoud, na Amrullah Saleh, naibu rais wa serikali iliyotimiliwa, ambaye ni hasimu mkubwa wa Taliban na ambaye alikimbilia Panjshir.

Taliban yaahidi kulinda wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada

Siku ya Jumapili Taliban waliahidi kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada na kuwezesha misaada kuingia nchini Afghanistan wakati wa mkutano na afisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema. Martin Griffiths, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu, alikuwa ziarani huko Kabul Jumapili (Septemba 5) kwa mazungumzo na viongozi wa Taliban wakati nchi hiyo inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.