Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Taliban yatoa ahadi mpya kwa Marekani kuhusu uokoaji

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, leo Jumanne, amepewa ahadi mpya kutoka kwa Taliban ya kuwaruhusu Waafghan ambao wanataka kuondoka nchini. Hilo litafanya bila kizuizi, amesema Antony Blinken akinukuu viongozi wa Taliban baada ya  kukutana nao katika wa ziara yake ya kiserikali nchini Qatar.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (wapili kutoka kulia) na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin (kushoto) akiwa na Naibu Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya nje Mohammed bin Abdulrahman Al Thani (kulia).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (wapili kutoka kulia) na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin (kushoto) akiwa na Naibu Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya nje Mohammed bin Abdulrahman Al Thani (kulia). Olivier DOULIERY POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Qatar kwa upande wake imethibitisha kwamba uwanja wa ndege wa Kabul utafunguliwa hivi karibuni, bila kutoa tarehe.

Antony Blinken, akiambatana na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba amepokea ahadi mpya kutoka kwa viongozi wapya wa Afghanistan kwamba "watawaruhusu watu wenye hati za kusafiri kuondoka bila kizuizi."

"Tunawasubiri juu ya suala hili," ameongeza. "Jumuiya nzima ya kimataifa inasubiri Taliban kuheshimu ahadi hii."

Utawala wa Joe Biden unakabiliwa na shinikizo dhidi ya taarifa wakati mwingine za kutatanisha juu ya watu mia kadhaa, ikiwa ni pamoja na Wamarekani, ambao wamekwama katika uwanja wa ndege wa Mazar-i-Sharif kaskazini mwa Afghanistan, kulingana na Marina LeGree, mkurugenzi wa shirika lilisilo la kiserikali la Ascend Athletics, kutoka Marekani.

Kati ya watu 600 na 1,300 kwa jumla wanajaribu kuondoka Afghanistan, ikiwa ni pamoja na Wamarekani 19, kwa msaada wa shirika lake na mashirika mengine, amesema.

Kwa suala hili, Bwana Blinken ameeleza kuwa Taliban haikuzuia mtu yeyote kuondoka na vyeti halali vya kusafiri, lakini kwamba sio abiria wote ambao wana vyeti hivyo. Hakuna "watu waliotekwa nyara" huko Mazar-i-Sharif, amebaini, akisema kwamba hakuna maafisa wa Marekani katika eneo hilo.

"Hatuko katika nafasi ya kudhibitisha ukweli wa orodha za abiria, kutambua abiria waliomo kwenye ndege hizi, itifaki za usalama, au mahali ambapo ndege zinakusudia kutua. Huu ni wasiwasi kweli.", Ameeleza . "Tunajadili ninapozungumza na wewe kutatua maswali haya."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.