Pata taarifa kuu
MAREKANI-USHIRIKIANO

Washington yalegeza vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi ya Taliban

Ili kuwezesha kusafirisha misaada ya kibinadamu nchini Afghanistan, Washington imeamua kulegeza vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi ya Taliban. Kuna dharura, mamilioni ya Waafghan wanahitaji msaada wa kimataifa wa kibinadamu ili kuishi na nchi inakabiliwa na mdororo wa kiuchumi kutokana na vikwazo vya kimataifa.

Nusu ya watu wa Afghanistan kwa sasa wanategemea misaada ya kibinadamu. Kabul, Septemba 24, 2021.
Nusu ya watu wa Afghanistan kwa sasa wanategemea misaada ya kibinadamu. Kabul, Septemba 24, 2021. dpa/picture alliance via Getty I - picture alliance
Matangazo ya kibiashara

Msamaha wa kwanza unaruhusu serikali ya Marekani, mashiriki yasiyo ya kiserikali, baadhi ya mashirika na mashirika ya kimataifa kutoa msaada wa kibinadamu kwa Afghanistan. Washington pia imeidhinisha kusafirisha kwenda Afghanistan kwa bidhaa za kilimo, dawa na vifaa vya matibabu. Kwa upande mwingine, Marekani bado inazuia akiba ya Benki Kuu ya Afghanistan.

Misamaha hii ni ya haraka. Wakati wa baridi unakaribia, Afghanistan iliyokumbwa na mdororo wa kiuchumi iko katika hatari ya kutumbukia kwenye mgogoro mkubwa wa kibinadamu bila msaada wa kimataifa. Tangu Taliban ichukue madaraka, mipango kadhaa ya kibinadamu imesitishwa na ufadhili wa kigeni umekatwa, ikiwa ni pamoja na ufadhili kutoka Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, nusu ya wakaazi wa Afghanistan, sawa na watu milioni 18, wanategemea msaada wa kimataifa ya kibinadamu. Chini ya shinikizo la Umoja wa Mataifa, jamii ya kimataifa mwezi huu iliahidi karibu bilioni 1 ya msaada kwa Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.