Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Taliban yashtumiwa tena kuua raia

Nasir Ahmad Andisha, balozi wa serikali ya zamani ya Afghanistan katika Umoja wa Mataifa, ametoa wito wa kuchunguza tena ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na Taliban. Wiki iliyopita, Baraza la Haki za Binadamu lilishutumu mamlaka mpya ya Afghanistan kwa kuzidi kutumia vurugu ili kutuliza maandamano. Kulingana na BBC, Taliban wamewaua raia 20 huko Panshir.

Balozi wa zamani wa Afghanistan kwenye Umoja wa Mataifa Nasir Ahmad Andisha wakati wa hotuba yake huko Geneva, Uswisi, Agosti 24, 2021.
Balozi wa zamani wa Afghanistan kwenye Umoja wa Mataifa Nasir Ahmad Andisha wakati wa hotuba yake huko Geneva, Uswisi, Agosti 24, 2021. REUTERS - DENIS BALIBOUSE
Matangazo ya kibiashara

Katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii na ambayo sehemu yake ilirekodiwa na BBC Jumatatu, Septemba 13, inaonesha mpita njia akizungukwa na Taliban, akipelekwa kando ya barabara na kuuawa, wakati raia hyo akisema: yeye sio askari , licha ya sare za jeshi ambayo amevaa. Ni utaratibu wa kawaida wa kuvaa katika bonde la Panshir, ameelezea mwandishi wa habari.

Kituo hiki cha Uingereza kinasema angalau raia 20 wameuawa katika eneo hilo tangu Taliban ilipochukuwa udhibiti wa mji lkuu wa Afghanistan, Kabul mwezi Agosti 2021. Na BBC imetoa jina la mmoja wa wahanga, kwa ombi la familia yake: Abdul Sami, mfanyabiashara anayetuhumiwa kuuza SIM kadi kwa wapiganaji wa upinzani waliokamatwa na Taliban. Kulingana na mashuhuda, mwili wake, uliotupwa siku chache baadaye mbele ya nyumba yake, ulikuwa na majeraha kana kwamba aliteswa kabla ya kuuawa. Panshir lilikuwa jimbo la mwisho lililokuwa mikononi mwa upinzani baada ya ushindi wa Taliban. Hata hivyo Taliban wanakanusha kuhusika na mauaji yoyote ya raia.

Lakini habari juu ya unyanyasaji uliofanywa na Taliban inaendelea kusambaa. Jumatatu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet, alielezea kwamba alipokea shutuma za kuaminika za mauaji ya wanajeshi wa zamani wa Afghanistan na 'kukamatwa kwa raia waliofanya kazi kwa tawala zilizopita na familia zao. Hii inakuja licha ya Taliban kudai mara kwa mara kwamba wote wamepewa msamaha.

"Mamilioni ya watu wanahofia maisha yao na kuminywa kwa haki zao"

Nasir Ahmad Andisha, balozi wa zamani wa haki za binadamu wa serikali ya Afghanistan, alitoa wito kwa Umoja wa MAtaifa kuchunguza mara moja vurugu za Taliban. Baada ya kutoa wito kama huo Agosti 24, bila mafanikio, Hivi sasa anajaribu tena kupaza sauti ili aweze kusikika.

"Tofauti na matumaini ya tahadhari yaliyokuwepo, hali ya Afghanistan inaendelea kuzorota chini ya utawala wa Taliban, " alisema.

Leo hii ulimwengu hauwezi na haupaswi kukaa kimya, kwani mamilioni ya watu wanahofia maisha yao na haki zao na mzozo wa kibinadamu unajitokeza nchini. Wanawake na wasichana wako katika hatari zaidi.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.