Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Wanawake waandamana kutetea haki zao

Baada ya tangazo la Taliban juu ya serikali ya mpito inayojumuisha wajumbe wa Taliban na bila wanawake, mamia ya waandamani walimiminika mitaani Jumatano wiki hii, wakionyesha hasira zao. Wanawake ni miongoni mwa waandamanaji hao.

Wanawake wakiandamana huko Kabul mnamo Septemba 7, 2021.
Wanawake wakiandamana huko Kabul mnamo Septemba 7, 2021. AP - Wali Sabawoon
Matangazo ya kibiashara

Mina ameshiriki katika maandamano kadhaa ambayo yamefanyika katika mji wa Kabul dhidi ya Taliban katika siku za hivi karibuni. "Sikuogopa mara ya kwanza na Taliban hawakutuzuia siku hiyo," anasema. Lakini niliogopa mara ya pili wakati Taliban ilianza kuwapiga wanawake na kurusha mabomu ya machozi. Nilimwona mwanamke mmoja aliyejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa kichwani waya ya umeme na askari wa Taliban. Walitutendea vibaya, wakatuita makahaba, na wakasema tunaungwa mkono na Marekani. "

Wakati huo huo Marekani na Ujerumani zimewatakaTaliban iruhusu ndege za kukodisha zisafirishe watu kutoka uwanja wa Kabul. Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas na mwenzake wa Marekani Antony Blinken wametoa wito huo baada ya mazungumzo yao kwenye kituo cha jeshi la anga la Marekani cha Ramstein kilichopo kwenye jimbo la Rhineland-Palatinate la kusini magharibi mwa Ujerumani.

Mawaziri hao wawili walifanya mazungumzo kabla ya mkutano kwa njia ya Video, na mawaziri wengine wa mambo ya nje wa nchi za jumuiya ya kijeshi ya NATO pamoja na katibu mkuu wa jumuiya hiyo bwana Jens Stoltenberg.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.