Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Taliban yasambaratisha maandamano ya wanawake Kabul

Wanawake sita wa Afghanistan wamejaribu kwa muda mfupi Alhamisi hii asubuhi kuandamana huko Kabul kudai haki yao ya elimu, kabla ya kuzuiwa kwa nguvu na Taliban waliofyatua risasi hewani, waandishi wa habari wa AFP wameibaini.

Afisa wa Taliban azungumza na waandamanaji nje ya shule huko Kabul, wakati mwingine anajaribu kumzuia mwandishi wa habari asipige picha.
Afisa wa Taliban azungumza na waandamanaji nje ya shule huko Kabul, wakati mwingine anajaribu kumzuia mwandishi wa habari asipige picha. © AFP/BULENT KILIC
Matangazo ya kibiashara

Karibu saa 8:00 asubuhi, saa za Afghanistan, wasichana watatu waliovaa hijabu na barakoa wakibebelea bango lililoandikwa kwa Kingereza: "Elimu isiingizwe katika siasa!" wameandamana mbele ya shule ya upili ya wasichana ya Rabia Balkhi, mashariki mwa mji mkuu wa Afghanistan.

"Msivunje kalamu zetu, msichome vitabu vyetu, umsifunge shule zetu," maneno ambayo yameandikwa kwenye mabango yaliyokuwa yakibebwa na waandamanaji hao.

Mara tu walipojiunga na waandamanaji wengine watatu, mmoja wao akiwa amebeba bango ambalo lilikuwa limeandikwa "Elimu ni kitambulisho cha mwanadamu", wapiganaji kadhaa wa Taliban waliwasili na kuanza kuwarejesha nyuma waandamanaji hao kuelekea mlango wa kuingilia na kutoka shuleni. Mmoja wao walijieleleza kwa waandishi wa habari wa kigeni na kujaribu kuwazuia wasifanye kazi yao.

"Ninawaheshimu hayakuruhusiwa," amesema mkuu wa wapiganaji hao wa Taliban katika mji wa Kabul. "Mamlaka ya Ufalme wa (Kiislamu) ya Afghanistan ilikuwa haijapewa taarifa. Hii ndio sababu hakuna waandishi wa habari wa Afghanistan wako hapa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.