Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI

Suhail Shaheen: 'Hakuna atakayenufaika na kudhoofika kwa Afghanistan'

Kiongozi wa mazungumzo na msemaji wa Taliban Suhail Shaheen amefanya mahojiano na RFI huko Doha, nchini Qatar. Utawala wa Kabul umemteua kuwa balozi wa Afghanistan katika Umoja wa Mataifa, hatua ambayo haina nguvu yoyote wakati huu kwa sababu ya kutotambuliwa kimataifa.

Suhail Shaheen, kiongozi wa mazungumzo na msemaji wa Taliban.
Suhail Shaheen, kiongozi wa mazungumzo na msemaji wa Taliban. © RFI/Nicolas Falez
Matangazo ya kibiashara

Suhail Shaheen amezungumzia mazungumzo yanayoshindikana kati ya Taliban na nchi za Magharibi, hali ya wanawake na jamii ya watu walio wachache na tishio la kundi la islamic State nchini Afghanistan.

Akihojia na RFI kuhusu mazungumzo kati ujumbe wa Taliba na wawakilishi wa Marekani na Ulaya, Suhail Shaheen amesema "maendeleo ya kwanza ni kwamba kila upande umegundua kuwa ni bora kuzungumza, kutatua shida kupitia majadiliano na uelewa. Na kila upande ulielewa kuwa shinikizo halikuwahi kuwa nafasi na wala halina nafasi kwa sasa. Kwa hivyo, ni bora kuelewana, kuleta maswala yote kwenye meza ya mazungumzo kuyajadili na kupendekeza njia za kuyasuluhisha. Kwa kweli, huwezi kutatua shida zote katika mkutano mmoja. Lakini, pande zote mbili, kila mtu alikubali kuendelea na mikutano kama hii".

Amebaini kwamba serikali ya sasa ya Afghanistan inapaswa kutambuliwa kimataifa. Kwa sababu tuna udhibiti wa mipaka yetu yote, tuna uhuru wa nchi yetu, tunaungwa mkono na raia wa Afghanistan. Hizi ndizo kanuni za msingi ambazo serikali inatambuliwa. Utawala wa zamani huko Kabul hautumii tena mamlaka juu ya sehemu yoyote ya nchi, kwa hivyo hawawakilishi mtu yeyote, ameongeza.

Tuna imani kuwa tutatambuliwa. Tunataka kufanya mazungumzo na Umoja wa Mataifa, na nchi zingine. Kwa sababu hali nzito inakuja na kuna masuala mengi ambayo yanahitaji ushirikiano, kama misaada ya kibinadamu na maswala mengine ambayo yanaweza kutokea ambayo yanaweza kutatuliwa kwa kuzungumza na kuelewana

.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.