Pata taarifa kuu

Mjumbe wa Marekani kwa Afghanistan Zalmay Khalilzad ajiuzulu

Mjumbe maalumu wa Marekani kwa Afghanistan Zalmay Khalilzad, ishara ya kutofaulu kwa Marekani dhidi ya Taliban, ameachia ngazi kwenye wadhifa wake, waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, ametangaza.

Bw. Khalilzad amekuwa akihudumu kama mjumbe maalumu wa upatanishi katika tawala za Trump na Biden tangu Septemba 2018, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo Mike Pompeo kumpa nafasi ya kuongoza timu ya usuluhishi kati ya serikali ya Afghanistan na wanamgambo wa Taliban.
Bw. Khalilzad amekuwa akihudumu kama mjumbe maalumu wa upatanishi katika tawala za Trump na Biden tangu Septemba 2018, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo Mike Pompeo kumpa nafasi ya kuongoza timu ya usuluhishi kati ya serikali ya Afghanistan na wanamgambo wa Taliban. AP - Jose Luis Magana
Matangazo ya kibiashara

Zalmay Khalilzad alikuwa anashikilia nafasi hii tangu 2018. Kwa sasa nafasi hiyo inachukuliwa na naibu wake Thomas West, ambaye alikuwa mshauri wa Ikulu ya White House wakati Joe Biden alikuwa makamu wa rais chini ya utawala wa Barack Obama, ameema Antony Blinken katika taarifa fupi.

Bw. Khalilzad amekuwa akihudumu kama mjumbe maalumu wa upatanishi katika tawala za Trump na Biden tangu Septemba 2018, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo Mike Pompeo kumpa nafasi ya kuongoza timu ya usuluhishi kati ya serikali ya Afghanistan na wanamgambo wa Taliban.

Awali Zalmay Khalilzad alipanga kujiuzulu katika wadhfa huo mwezi Mei baada ya rais Biden kutangaza kuyaondoa kabisa majeshi ya Marekani kabla ya kumbukumbu ya miaka 20 mashambulizi ya 9/11, lakini aliombwa asalie na akanafanya hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.