Pata taarifa kuu

Marekani haitashiriki kwenye mazungumzo ya Afghanistan Moscow

Marekani imetangaza kwamba haitashiriki mazungumzo kuhusu Afghanistan yaliyopangwa kufayika leo Jumanne huko Moscow na ambayo Urusi, China na Pakistan zitashiriki.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price. REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

"Tutafurahi kushiriki kongamano hili siku za usoni, lakini hatuwezi kushiriki katika kikao hiki wiki hii," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amewaambia waandishi wa habari.

Mikutano hii "imekuwa na ufanisi hapo zamani. Ni ngumu kwetu kushiriki kikao hicho wiki hii ”, Ned Price amebainisha bila kutoa maelezo zaidi. Urusi itakuwa itapokea ujumbe wa Taliban huko Moscow Oktoba 20. Siku moja kabla, alitaka kufikia msimamo wa pamoja juu ya suala la Afghanistan kwa ushirikiano na China, Pakistan na Marekani.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ana wasiwasi juu ya matamanio ya kundi la Islamc State nchini Afghanistan, akioghofia kuwamba eneo lote upande wa kusini mwa Urusi linaweza kukumbwa na mdororo wa usalama. Islamic State-Khorasan (IS-K), kundi la itikadi kali lenye silaha nchini Afghanistan, hivi karibuni lilidai kuhusika na mfululizo wa mashambulizi yaliyokusudiwa kuhatarisha usalama wa "emirate" jina lililochukuwa nafasi ya Afghanistan, lililotangazwa na Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.