Pata taarifa kuu
IRAN

Washington yakanusha kubadilishana wafungwa na Tehran

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imekanusha habari za kubadilishana wafungwa na Iran, wakati Tehran imethibitisha tangazo la runinga ya Lebanon likibaini kuepo kwa zoezi la kubadilishana wafungwa ambalo linaendelea.

Iran na nchi zenye nguvu duniani  hivi sasa ziko katika mazungumzo kujaribu kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 ambayo Washington iliajiondoa miaka mitatu iliyopita wakati wa utawala wa Donald Trump.
Iran na nchi zenye nguvu duniani hivi sasa ziko katika mazungumzo kujaribu kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 ambayo Washington iliajiondoa miaka mitatu iliyopita wakati wa utawala wa Donald Trump. via REUTERS - EU DELEGATION IN VIENNA
Matangazo ya kibiashara

"Habari zinazoeleza kuhusu kufikiwa kwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa sio kweli," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya MArekani Ned Price ameliambia shirika la habari la REUTERS. "Kama tulivyosema, kila wakati tunashughulikia kesi za Wamarekani waliowekwa kizuizini au kupotea nchini Iran. Hatutachoka hadi tuweze kuwaunganisha na familia zao."

Hapo awali, televisheni ya serikali ya Irani, ikinukuu afisa mmoja, ilithibitisha ripoti kutoka kituo cha televisheni kinachounga mkono Iran cha Al Mayadeen kwamba Iran itawaachilia Wamarekani wanne wanaotuhumiwa kwa ujasusi huku Marekani ikiwaachilia raia wanne wa Iran wanaozuiliwa nchini Marekani.

Huko London, afisa wa Wizara ya Mambo ya nje ya Uingereza, kwa upande wake, alipuuzia madai kuhusu uwezekano wa kuachiliwa kwa raia wa UIngereza mwenye asili ya Iran anayefanya kazi katika shirika la kutoa misaada la Nazanin Zaghari-Ratcliffe.

Televisheni ya serikali ya Iran ilimnukuu afisa wa Iran akisema kwamba ataachiliwa "baada ya malipoya deni la kijeshi" ambalo Uingereza inadaiwa na Tehran.

Iran na nchi zenye nguvu duniani  hivi sasa ziko katika mazungumzo kujaribu kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 ambayo Washington iliajiondoa miaka mitatu iliyopita wakati wa utawala wa Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.