Pata taarifa kuu
AUSTRIA

Mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kuanza tena Vienna

Mazungumzo ya kuokoa mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yalimalizika wiki iliyopita huko Vienna kwa hatua nzuri. Wawakilishi wa nchi zilizosaini mkataba huo wanaendelea tena leo Alhamisi, lakini wakati huo huo, uamuzi wa Tehran kuimarisha uranium hadi 60% umesababisha hali ya kutoelewana.

Mlango wa Hoteli ambapo mazungumzo mapya kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yalifanyika, Aprili 6, 2021 huko Vienna, Austria.
Mlango wa Hoteli ambapo mazungumzo mapya kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yalifanyika, Aprili 6, 2021 huko Vienna, Austria. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa kukaribia 90% kiwango muhimu kwa matumizi ya kijeshi, Jamhuri ya Kiislamu "imeweka shinikizo kwa kila mtu", amebaini mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya.

Baada ya kuanza vizuri, "ni kweli kwamba hali hii inafanya mambo kuwa magumu", mwanadilpomasia huyo ameliambia shirika la habari la AFP kabla ya mkutano mpya wa pande zinazohusika na mkataba huyo (Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, China, Urusi na Iran), uliopangwa kufanyika saa 6:30 mchana. saa za Austria (sawa na saa 10:30 asubuhi sasa za kimataifa).

Awali Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zilielezea "wasiwasi wao mkubwa" juu ya nia ya Iran ya kuongeza urutubishaji wa uranium hadi 60% katika kituo chake cha nyuklia cha Natanz.

Mkataba wa mwaka 2015, JCPOA, ulifikiwa kati ya Iran na wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Ufaransa, wanaojulikana kama “P5+1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.