Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI

Mazungumzo ya nyuklia ya Iran kuanza tena Ijumaa

Mazungumzo yasio ya  moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yenye lengo la kuzileta pamoja pande hizo mbili kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran wa 2015 yataanza tena siku ya Ijumaa wiki ijayo, mkuu wa ujumbe wa Urusi amesema Jumamosi hii.

Mikhail Ulyanov, mkuu wa ujumbe wa Urusi katika mazungumzo kati ya Marekani na Iran.
Mikhail Ulyanov, mkuu wa ujumbe wa Urusi katika mazungumzo kati ya Marekani na Iran. REUTERS - LEONHARD FOEGER
Matangazo ya kibiashara

Mikhail Ulyanov, balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, amewaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yanaendelea lakini kufikiwa kwa hatua kubwa ni kama ndoto.

Mazungumzo yamekuwa yakifanyika tangu mapema mwezi Aprili huko Vienna kujaribu kushawishi Marekani na Iran kuheshimu mkataab huo, ambao chini ya utawala wa Donald Trump Marekani ilijiondoa mnamo mwaka wa 2018 na ambapo Iran imekuwa ikijiondoa hatua kwa hatua tangu wakati huo.

Umoja wa Ulaya unachukua nafasi ya mpatanishi katika mazungumzo haya ambayo China, Urusi, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zinashiriki - ambazo zote zilitia saini kwenye mkataba huo unaoitwa Mpango wa Utekelezaji wa Pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.