Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USALAMA

Mauaji ya Mkorea Kusini: Pyongyang yaonya jeshi la wanamaji la Korea Kusini

Korea Kaskazini imeomba jeshi la wanamaji la Korea Kusini kukoma kuingia katika maji yake ya baharini, wakati Seoul inatafuta mwili wa afisa wa Korea Kusini aliyepigwa risasi baharini na wanajeshi wa Korea Kaskazini.

Wakorea Kusini wakitazama picha za kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kwenye kwenye televisheni katika kituo cha treni cha Seoul Septemba 25, 2020.
Wakorea Kusini wakitazama picha za kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kwenye kwenye televisheni katika kituo cha treni cha Seoul Septemba 25, 2020. AFP
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari vya serikali vya Korea Kaskazini vmeripoti kuwa Pyongyang itaanza zoezi la kutafuta mwili huo, na kubaini kwamba shughuli za Korea Kusini zinaweza kuhatarisha kuongezeka kwa mivutano.

Afisa katika tasnia ya uvuvi ya Korea Kusini aliuawa kwa kupigwa risasi na askari wa Korea Kaskazini siku ya Jumanne. Hii ni mara ya kwanza kwa muongo mmoja raia wa Korea Kusini anauawa kwa njia kama hii.

Kim Jong Un aliomba msamaha siku ya Ijumaa baada ya kifo "cha fedheha", kulingana na Seoul, akitaka kumtuliza jirani yake wa kusini ambapo mauaji hayo yalizua hasira miongoni mwa raia wa Korea Ksini.

Maafisa wa jeshi la Korea Kusini wanasema kwamba mtu huyo alihojiwa akiwa katika baharini kabla ya kuuawa kwa "amri ya afisa wa juu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.