Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USALAMA

Pyongyang kuongeza idadi ya askari wake karibu na eneo la mpaka wa Korea mbili

Pyongyang imetishia kuongeza idadi ya askari wake karibu na eneo la mpaka wa Korea mbili (DMZ) baada ya kuripua ofisi ya pamoja na Korea Kusini, wakati mvutano ukiendelea kuongezeka kati ya nchi hizo mbili jirani.

Korea Kaskazini yaendelea na vitisho dhidi ya Korea Kusini.
Korea Kaskazini yaendelea na vitisho dhidi ya Korea Kusini. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kitendo cha Korea Kaskazini kuripua ofisi ya pamoja na Korea Kusini kililaaniwa na Seoul.

Korea Kaskazini pia imesema imefutilia mbali ombi lililotolewa na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in la kutuma wajumbe kwa mazungumzo.

Kim Yo Jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, mwenye ushawishi mkubwa katika taifa hilo, anaona ni "pendekezo lisilokuwa na umuhimu wowote na halina muelekeo", kulingana na shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA.

"Tunaonya kuwa hatutavumilia tena vitendo na maneno yasiyo na maana kutoka Korea Kaskazini," amesema msemaji wa Blue House, ikulu ya rais wa Korea Kusini, Yoon Do-han

Kwa upande wake, Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imebaini kwamba vitisho kutoka Korea Kaskazini vitakiuka makubaliano kadhaa yaliyofikiwa kati ya Korea hizo mbili ikiwa vitatekelezwa. "Korea Kaskazini itajutia ikiwa vitisho hivyo vitatekelezwa," Wizara ya Ulinzi imesema katika taarifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.