Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USALAMA

Pyongyang yaishtumu Seoul kwa kufanya mazoezi ya kijeshi

Korea Kaskazini imeinyooshea kidole cha lawama Korea Kusini kufanya mazoezi ya kijeshi mapema wiki hii, mwakilishi wa jeshi la Pyongyang akinukuliwa na vyombo vya habari vya Korea Kaskazini amekiita kitendo hicho kama "uchokozi mkubwa" akitoa wito wa kuchukuwa hatua.

Kiongozi wa Kikorea Kaskazini Kim Jong-un, amezungukwa na maveterani katika jeshi la nchi hiyo, picha hii iliyotolewa Julai 27, 2018 na serikali ya Pyongyang.
Kiongozi wa Kikorea Kaskazini Kim Jong-un, amezungukwa na maveterani katika jeshi la nchi hiyo, picha hii iliyotolewa Julai 27, 2018 na serikali ya Pyongyang. KCNA via REUTERS ATTENTION EDITORS
Matangazo ya kibiashara

"Mazoezi haya ya hivi karibuni yanatuwezesha mara nyingine kujuwa kuwa ni dhahiri kwamba maadui watabaki kuwa maadui kila wakati," mwakilishi wa jeshi la Korea Kaskazini amesema katika taarifa iliyotolewa na shirika la habari la KCNA.

Pyongyang inalaani mazoezi ya kijeshi ya Korea Kusini iliyofanya Jumatano wiki hii, na kuyataja kinyume na makubaliano kati ya Korea mbili yanayokusudia kupunguza mvutano kati ya Kaskazini na Kusini.

"Hali inarudi kwenye hatua ya kwanza, kabla ya mkutano wa kilele wa Korea Kusini wa mwaka 2018," imeandika katika taarifa.

Taarifa hizi zinakuja siku tano baada ya Korea Kaskazini na Korea Kusini kufyatuliana risasi kwenye mpaka kati ya hizo mbili. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo. Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo alisma kuwa risasi hizo zilifyatuliwa kimakosa.

Katika taarifa tofauti, KCNA ilisema kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alituma ujumbe wa sauti kwa rais wa China Xi Jinping kumpongeza kwa kudhibiti mgogoro wa kiafya ya Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.