Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Korea Kaskazini yarusha makombora kuelekea bahari ya Japan

Korea Kaskazini imerusha makombora kadhaa kuelekea katika Bahari ya Japan au katika Bahari ya Mashariki Jumanne wiki hii, jeshi la Korea Kusini limesema.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un alidai kuwa nchi yake ina "silaha ya kimkakati".
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un alidai kuwa nchi yake ina "silaha ya kimkakati". STR / KCNA VIA KNS / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Makombora kadhaa" ambayo yanasemekana ni "makombora ya masafa mafupi" yamerushwa kutoka mji wa Munchon, Mashariki mwa nchi, makao makuu ya jeshi la Korea Kusini yamesema katika taarifa.

Majarabio hayo yanakuja wakati Korea Kaskazini inajianda kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa ya miaka 108 ya mwanzilishi wa utawala wa nchi hiyo, Kim Il Sung, babu wa kiongozi wa sasa Kim Jong Un, na pia Korea Kusini inajiandaa kufanya uchaguzi wa wabunge.

Majaribio hayo yamefanyika wakati jumuiya ya kimataifa inaendelea na vita dhidi ya janga la Covid-19. Pyongyang inadai kuwa haina kesi yoyote ya maambukizi ya maambukizi yanayo sababisha ugonjwa hatari wa Covid-19.

Katika miaka ya hivi karibuni, Korea Kaskazini, nchi ambayo inadaiwa kuwa na bomu la atomiki, ilirusha makombora mengi ya masafa marefu, makombora mengine mengi, huku Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zikiona kuwa ni kitisho cha Korea Kaskazini kwa ulimwengu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.