Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI- KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Kim asimamia zoezi la kurusha makombora ya masafa marefu

Korea Kaskazini inaendelea na mpango wake wa kurusha makombora ya masafa marefu, baada ya mazungumzo na Marekani kusimama kwa muda mrefu.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anadai kuwa nchi yake ina "silaha mpya ya kimkakati".
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un anadai kuwa nchi yake ina "silaha mpya ya kimkakati". STR / KCNA VIA KNS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alisimamia zoezi la kurusha makombora ya masafa marefu, shirika la habari la la serikali KCNA limeripoti leo Jumanne.

Tangazo hilo linakuja baada ya Korea Kusini kubaini Jumatatu kwamba Korea Kaskazini siku ya Jumatatu ilifanya majaribio ya makombora mawili ya masafa mafupi kutoka pwani yake ya Kusini kuelekea baharini.

Picha zilizotolewa na vyombo vya habari vya serikali huko Pyongyang zinaonyesha wanajeshi wa Korea Kaskazini wakijaribu kutumia bunduki kubwa ya kurusha roketi nyingi, banduki iliyonekana kwa mara ya kwanza mwaka jana.

Januari 1, Kim alisema kwamba nchi yake inataka kuendelea kuimarisha mpango wa nyuklia wa nchi yake na kuzindua katika siku za usoni "silaha mpya ya mkakati", baada ya kushindwa kuanza tena kwa mazungumzo na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.