Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI-USALAMA

Korea Kaskazini yaripua ofisi ya pamoja na Korea Kusini

Jumanne hii, Juni 16, Korea Kaskazini imeharibu ofisi ya pamoja na korea Kusini huko Kaesong, mji ulio karibu na mpaka, Wizara ya ushirikiano ya Korea Kusini imetangaza, siku kadhaa baada ya Pyongyang kutoa maneno makali.

Ofisi hiyo ilifunguliwa mwezi Septemba 2018 kama sehemu ya makubaliano kati ya kiongozi wa kaskazini Kim Jong Un na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini.
Ofisi hiyo ilifunguliwa mwezi Septemba 2018 kama sehemu ya makubaliano kati ya kiongozi wa kaskazini Kim Jong Un na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini. Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Korea Kaskazini imeripua ofisi ya pamoja ya Kaesong saa 2:49 mchana, " msemaji wa wizara ya ushirikiano kati ya Korea Kusini na Kaskazini ametangaza katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Ofisi hiyo ilifunguliwa mwezi Septemba 2018 kama sehemu ya makubaliano kati ya kiongozi wa kaskazini Kim Jong Un na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini.

Wakati huo huo Korea Kaskazini imesema inaliweka jeshi lake kwenye hali ya kivita, ikiituhumu jirani yake Korea Kusini kuruhusu wanaharakati kurusha maputo yenye ujumbe wa uchochezi kuelekea Kaskazini.

Mkuu wa jeshi la Korea Kaskazini amesema wanaandaa mpango mkakati wa kuingia maeneo ambayo yaligeuzwa kuwa yasiyo na shughuli za kijeshi mwaka 2018, akitishia kuyageuza magofu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.