Pata taarifa kuu

Mikutano ya Trump/Kim: Seoul yamtuhumu Bolton kwa 'kupotosha' ukweli katika kitabu chake

Ikulu ya rais ya Korea Kusini leo Jumatatu imemtuhumu mshauri wa zamani wa usalama wa kitaifa wa Marekani John Bolton kwa "kupotosha" ukweli katika nakala ya kitabu chake cha mchakato wa kidiplomasia na Pyongyang.

Mshauri wa zamani wa usalama wa kitaifa wa Donald Trump John Bolton na Rais wa Marekani katika Ikulu ya White House tarehe 9 Aprili, 2018.
Mshauri wa zamani wa usalama wa kitaifa wa Donald Trump John Bolton na Rais wa Marekani katika Ikulu ya White House tarehe 9 Aprili, 2018. MARK WILSON / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa usalama wa Bwana Moon, Chung Eui-yong, mtu ambaye alimwambia Bw. Trump kwamba Bw.Kim alitaka kuonana naye, na ambaye anayetajwa mara kadhaa kwenye kitabu hicho, amebaini kwamba kitabu hicho "hakielezi" ukweli sahihi "na kwamba" sehemu kubwa imepotosha ukweli wa mambo".

Hajatoa mifano hai kwa ukosoaji huu, lakini ameongeza kwamba kutolewa kwa maelezo juu mazungumzo ya nyuklia ya nchi mbili ni "kukiuka kanuni za msingi za masuala ya kidiplomasia na kuna nia mbaya ya kudhoofisha matunda yanayoweza kupatikana kwa pande zote na kwa majadiliano yajayo. "

"Sio sahihi kupotosha ukweli na kuwa na upendeleo," imesema Blue House, ikulu ya rais wa Korea Kusini katika taarifa.

Kwenye kitabu chake, Bwana Bolton anashtumu kukosekana kwa maandalizi ya Donald Trump kwa mkutano wake wa kwanza na Bw. Kim, mwezi Juni 2018 huko Singapore.

Pia amemshambulia Bwana Moon, akisema kwamba mchakato wote wa kidiplomasia ni "jitihada za Korea Kusini na hasa ambao unahusiana sana na ajenda yake ya" muungano "kuliko mkakati muhimu kutoka kwa Kim au Marekani. "

Ikulu ya rais Marekani ilikuwa inajarbu kuzuia kitabu kisitoke, lakini vyombo vya habari vya Marekani vilikuwa na nakala ambayo vilianza kuichapisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.