Pata taarifa kuu
MAREKANI-UHAMIAJI-TRUMP-HAKI

Wahamiaji: Donald Trump matatani baada ya mpango wake kukataliwa na mahakama ya juu

Wakati kampeni za uchaguzi nchini marekani zinaanza tena, rais Donald Trump ambaye anawania kiti cha urais kwa muhula wa pili, anaendelea kupoteza katika nyanja ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kiafya na kidiplomasia.

Rais aw Marekani Donald Trump katika mkutano katika Ikulu ya White House, Juni 18, 2020.
Rais aw Marekani Donald Trump katika mkutano katika Ikulu ya White House, Juni 18, 2020. REUTERS/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump ameendelea kujikuta katika hali ya sintofahamu. Alhamisi wiki hii Mahakama Kuu imelikataa jaribio lake kukomesha mpango, uliopewa jina la "Dreamers", unaowalinda dhidi ya kufukuzwa mamia kwa maelfu ya wahamiaji walioingia nchini Marekani kinyume cha sheria wakiwa watoto."

Majaji katika kura ya watano dhidi ya wanne, wamethibitisha hukumu ya mahakama ya chini, iliyobainisha kuwa hatua ya Trump ya mwaka 2017 kufuta mpango huo ulioanzishwa mwaka 2012 na mtangulizi wake Barack Obama, ilikuwa kinyume cha sheria.

Baadhi ya majaji wamegundua kwamba hatua za utawala wa Trump zilikuwa za kidhalimu na zisizotabirika chini ya sheria ya shirikisho inayojulikana kama sheria ya utaratibu wa kiutawala.

Rais Donald Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter akiushtumu uamuzi wa Mahakama ya Juu nchini Marekani.

"Mnaweza kuona jinsi gani Mahakama Kuu hainipendi, " ameandika rais Trump.

Hii ni mara ya pili ndani ya wiki moja Donald Trump akijikuta maamuzi yake yanafutiliwa mbali na mahakama ya juu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.