Pata taarifa kuu
MAREKANI-BERMAN-PHAKI

Aliyeendesha kesi dhidi ya washirika wa Trump akanusha kuwa amejiuzulu

Mwanasheria wa Marekani ambaye alisimamia mashitaka dhidi ya washirika wa karibu wa Rais Donald Trump wa Marekani, na uchunguzi dhidi ya wakili wake binafsi, Rudy Giulaini, amesema kuwa hana nia ya kujiuzulu baada ya Waziri wa Sheria kutangaza kuwa amejiuzulu.

Mwanasheria wa Wilaya ya Kusini mwa jimbo la New York Geoffrey Berman katika mkutano na waandishi wa habari huko New York Oktoba 10, 2019 (picha ya kumbukumbu)
Mwanasheria wa Wilaya ya Kusini mwa jimbo la New York Geoffrey Berman katika mkutano na waandishi wa habari huko New York Oktoba 10, 2019 (picha ya kumbukumbu) AFP
Matangazo ya kibiashara

Geoffrey Berman, mwendesha mashtaka tangu mwaka 2018 katika wilaya ya Kusini mwa jimbo la New York, alisimamia mashitaka ya Michael Cohen, wakili wa zamani wa Bw. Trump aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela mnamo mwezi Desemba 2018 kwa kusema uwongo katika Bunge la Congress, ambapo alidanganya kuhusu ushuru wake.

Awali Mwanasheria Mkuu wa Marekani, William Barr, katika taarifa yake, amesema kuwa Geoffrey Berman, anajiuzulu nafasi yake kama mwanasheria mkuu wa New York, na kwamba Trump amedhamiria kumteua mtu mwengine kuchukuwa nafasi hiyo, kuanzia tarehe 3 Julai.

Hakukutajwa sababu za Berman kujiuzulu ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu ashikilie nafasi hiyo, lakini tangazo hilo lilitolewa, baada ya Mwanasheria Mkuu Barr kukutana na maafisa wa polisi ya New York.

Kwa mujibu wa Barr, Trump atamteuwa mwenyekiti wa sasa wa kamisheni ya usalama, Jay Clayton, kushikilia nafasi ya Berman, ingawa wadadisi wanasema mwanasheria huyo hana uzoefu wowote wa ofisi ya mwendesha mashitaka wa serikali kuu.

Kuondoka kwa Berman kunakuja siku chache baada ya tuhuma za mshauri wa zamani wa masuala ya usalama wa Rais Trump, John Bolton, kwamba rais huyo alijaribu kuingilia uchunguzi uliokuwa ukifanywa na Berman juu ya Benki ya Halk ya Uturuki, katika jitihada za kusaka makubaliano na Rais Tayyip Erdogan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.